Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 3 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Novemba 2026

Jumanne · Juma la 31 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 31 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Martino wa Porres, mtawa · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Flp 2:5–11

5Muwe na nia kama aliyonayo Kristo Yesu. 6Ingawaje yeye ni sawa na Mungu. Lakini hakujali kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho. 7Badala yake, alijishusha mwenyewe. Alichukua umbo la mtumishi. Akajitokeza katika mfano wa wanadamu. Alionekana mwanadamu. 8Yeye alijinyeyekeza na kuwa mtii hadi kifo, kifo cha msalaba. 9Hivyo basi Mungu alimtukuza sana. Alimpa jina kuu lipitalo kila jina. 10Alifanya hivyo ili kwamba katika jina la Yesu kila goti sharti liiname. Magoti ya walio mbinguni na walio juu ya ardhi na chini ya ardhi. 11Na alifanya hivyo ili kwamba kila ulimi sharti ukiri kwamba Yesu kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Wimbo wa katikati

Zab 22:25–31

25Yahwe, katika kusanyiko la watu wako nitakusifu kwa yale uliyo tenda; nami nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wanao muhofu yeye. 26Walio onewa watakula na kutosheka; wale ambao humtafuta Yahwe watamsifu yeye. Mioyo yenu iishi milele. 27Watu wote wa duniani watakumbuka na kumrudia Yahwe; familia zote za mataifa watapiga magoti chini mbele yako. 28Kwa kuwa utawala ni wa Yahwe; yeye ni mtawala wa mataifa. 29Watu wote wa duniani waliofanikiwa wata sherekea na wata abudu; wale wote washukao katika mavumbi watapiga magoti mbele zake, wale ambao hawawezi kulinda maisha yao wenyewe. 30Kizazi kijacho kitamtumikia yeye; wao watakiambia kizazi kinachofuatia kuhusu Bwana. 31Wao watakuja na kuzungumza kuhusu haki yake; wao watawaambia watu ambao bado hawaja zaliwa yale ambayo Yahwe ameyafanya!

Injili

Lk 14:15–24

15Wakati mmoja wa wale walioketi mezani pamoja na Yesu aliposikia hayo, naye akamwambia, “Amebarikiwe yule atakayekula mkate katika Ufalme wa Mungu!” 16Lakini Yesu akamwambia, “Mtu mmoja aliandaa sherehe kubwa, akaalika watu wengi. 17Wakati sherehe ilipokuwa tayari, alimtuma mtumishi wake kuwaambia wale walioalikwa, 'Njooni, kwa sababu vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.' 18Wote, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi, 'Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali unisamehe.' 19Na mwingine akasema, 'Nimenunua jozi tano za ng'ombe, na mimi naenda kuwajaribu. Tafadhali uniwie radhi.' 20Na mtu mwingine akasema, 'Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.' 21Mtumishi akarudi na kumwambia bwana wake mambo hayo. Yule mwenye nyumba alikasirika akamwambia mtumishi wake, 'Nenda upesi mitaani na katika vichochoro vya mji ukawalete hapa maskini, vilema, vipofu na walemavu.” 22Mtumimishi akasema, 'Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa bado kuna nafasi.' 23Bwana akamwambia mtumishi, 'Nenda katika njia kuu na vichochoro na uwashurutishe watu waingie, ili nyumba yangu ijae. 24Kwamaana nawaambia, katika wale walioalikwa wa kwanza hapana atakayeonja sherehe yangu. '

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 3 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki