Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 2 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 2 Novemba 2026

Jumatatu · Juma la 31 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Kumbukumbu ya Marehemu Wote

Ukumbusho · Rangi ya liturujia: zambarau

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Omb 3:17–26

17Nafsi yangu imenyimwa amani; nimesahau furaha ni nini. 18Hivyo na sema, “Ustahimilivu wangu umeangamia na pia tumaini langu kwa Yahweh.” 19Kumbuka mateso yangu na kuangaika kwangu, maji machungu na uchungu. 20Ninaendelea kukumbuka na nimeinama ndani yangu. 21Lakini ni vuta hili akilini mwangu na hivyo nina matumaini: 22Upendo dhabiti wa Yahweh haukomi na huruma zake haziishi, 23ni mpya kila asubui; uaminifu wako ni mkubwa. 24“Yahweh ni urithi wangu,” Nilisema, hivyo nitamtumainia. 25Yahweh ni mwema kwao wanao msubiri, kwa anaye mtafuta. 26Ni vizuri kusubiri taratibu kwa uwokovu wa Yahweh.

Wimbo wa katikati

Zab 103:8, 10, 13–17

8Yahwe ni wa huruma na neema; ni mvumilivu; ana agano kuu la uaminifu. 10Hatushughulikii sisi kama dhambi zetu zinavyostahili au kutulipa kulingana na uhitaji wa dhambi zetu. 13Kama vile baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Yahwe alivyo na huruma kwao wamchao. 14Maana anajua tulivyo umbwa; anajua kuwa tu mavumbi. 15Kama ilivyo kwa mwanadamu, siku zake ni kama majani; hustawi kama ua katika shamba. 16Upepo hulipiga, nalo hutoweka, na hakuna hata mmoja awezaye kuelezea mahali lilipokua. 17Lakini agano la uaminifu wa Yahwe uko kwa wale wamchao yeye milele hata milele. Haki yake ni endelevu kwa uzao wao.

Somo la pili

1 Kor 15:51–57

51Tazama! Nawaambia ninyi siri ya kweli: Hatutakufa wote, bali wote tutabadilishwa. 52Tutabadilishwa katika wakati, katika kufumba na kufumbua kwa jicho, katika tarumbeta ya mwisho. Kwa kuwa tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa na hali ya kutoharibika, na tutabadilishwa. 53Kwani huu wa kuharibika lazima uvae wa kutoharibika, na huu wa kufa lazima uvae wa kutokufa. 54Lakini wakati huu wa kuharibika ukivikwa wa kutokuharibika, na huu wa kufa ukivaa wa kutokufa, ndipo utakuja msemo ambao umeandikwa, “Kifo kimemezwa katika ushindi.” 55“Kifo, ushindi wako uko wapi? Kifo, uko wapi uchungu wako?” 56Uchungu wa kifo ni dhambi, na nguvu ya dhambi ni sheria. 57Lakini shukurani kwa Mungu, atupaye sisi ushindi kupitia Bwana wetu Yesu Kristo!

Injili

Mt 11:25–30

au: Yn 12:23–26

25Katika muda huo Yesu alisema, “Nakusifu wewe, Baba, Bwana wa Mbingu na Nchi, kwa sababu uliwaficha mambo haya wenye hekima na ufahamu, na kuyafunua kwa wasio na elimu, kama watoto wadogo. 26Baba kwa kuwa ilikupendeza hivyo machoni pako. 27Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia. 28Njoni kwangu, nyinyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha. 29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu. 30Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.

Watakatifu wa 2 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki