Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 4 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 4 Novemba 2026

Jumatano · Juma la 31 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 31 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Karoli Borromeo, askofu · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Flp 2:12–18

12Kwa hiyo basi, wapendwa wangu kama mnavyotii siku zote, Si tu katika uwepo wangu lakini sasa ni zaidi sana hata pasipo uwepo wangu, uwajibikeni wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka. 13Kwa kuwa ni Mungu anayetenda kazi ndani yenu ili kuwawezesha kunia na kutenda mambo yale yampendezayo yeye. 14Fanyeni mambo yote bila malalamiko na mabishano. 15Fanyeni hivyo ili kwamba msilaumike na kuwa watoto wa Mungu waaminifu wasiyo na lawama. Fanyeni hivyo ili kwamba muwe nuru ya dunia, katika kizazi cha uasi na uovu. 16Shikani sana neno la uzima ili kwamba niwe na sababu ya kutukuza siku ya Kristo. Kisha nitafahamu kwamba sikupiga mbio bure wala sikutaabika bure. 17Lakini hata kama ninamiminwa kama sadaka juu ya dhabidhu na huduma ya imani yenu, ninafurahi, na ninafurahi pamoja nanyi nyote. 18Vilevile na ninyi pia mnafurahi, na mnafurahi pamoja nami.

Wimbo wa katikati

Zab 27:1, 4, 13–14

1Zaburi ya Daudi. Yahwe ni nuru yangu na wokovu wangu; nimuogope nani? Yahwe ni salama ya maisha yangu; ni mhofu nani? 4Kitu kimoja nimekiomba kwa Yahwe, nami nitakitafuta hicho: kwamba niweze kukaa katika nyumba ya Yahwe siku zote za maisha yangu, kuutazama uzuri wa Yahwe na kutafakari hekaruni mwake. 13Kitu gani kingeweza kunitokea kama nisingeamini kuwa nitauona uzuri wa Yahwe katika nchi ya walio hai? 14Umngoje Yahwe; uwe imara, na moyo wako uwe jasiri! Umngoje Yahwe!

Injili

Lk 14:25–33

25Sasa umati mkubwa walikuwa wanakwenda pamoja naye, naye akageuka na akawaambia, 26'Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, mama yake, mke wake, watoto wake, ndugu zake waume na wanawake- ndio, na hata maisha yake pia -hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 27Mtu asipochukua msalaba wake na kuja nyuma yangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo? 29Vinginevyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, wote walioona wataanza kumdhihaki, 30wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.' 31Au mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine katika vita, ambae hatakaa chini kwanza na kuchukua ushauri kuhusu kama ataweza, pamoja na watu elfu kumi kupigana na mfalme mwingine anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? 32Na kama sivyo, wakati jeshi la wengine bado liko mbali, hutuma balozi kutaka masharti ya amani. 33Kwa hiyo basi, yeyote kati yenu ambaye hataacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 4 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki