Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 2 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 2 Oktoba 2026

Ijumaa · Juma la 26 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 26 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Malaika Walinzi Watakatifu · Kumbukumbu

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ayu 38:1, 12–21; 40:3–4

1Ndipo Yahweh alimwita Ayubu kutoka katika dhoruba kali na kumwambia, 12Je tangu mwanzo wa siku zako, ulishawahi kuigiza asubuhi ianze, na kuyafanya mapambazuko yajue sehemu yake katika mpangilio wa vitu, 13ili kwamba ishikilie sehemu za dunia ili watu waovu watikiswe mbali nayo. 14Dunia imebadilishwa katika mwonekano kama udongo unavyobadilika chini ya muhuri; vitu vyote husimama juu yake dhahiri kama cha kibindo cha nguo. 15'Mwanga' wao umeondolewa kutoka kwa watu waovu; na mkono wao ulioinuliwa umevunjwa. 16Je umeshaenda kwenye vyanzo vya maji ya bahari? Je umeshatembea sehemu za chini kabisa za kilindi? 17Je malango ya mauti yamefunuliwa kwako? Je umeshaona malango ya uvuli wa mauti? 18Je umeifahamu dunia katika upana wake? Niambie kama unayajua yote hayo. 19Je iko wapi njia ya sehemu ya kupumzikia kwa mwanga, na kama ilivyo kwa giza, iko wapi sehemu yake? 20Je unaweza kuuongoza mwanga na giza katika sehemu zake za kazi? Waweza kuitambua njia ya kurudi katika nyumba zao? 21Bila shaka unajua, kwa kuwa ulizaliwa wakati huo; hesabu ya siku zako ni kubwa sana! 40:3Ndipo Ayubu akamjibu Yahweh na kusema, “ 4Tazama, mimi si mtu muhimu; je nawezaje kukujibu? Ninauweka mkono wangu juu ya mdomo wangu.

Wimbo wa katikati

Zab 139:1–3, 7–10, 13–14

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya daudi. Ee Yahwe, wewe umenichunguza, na unanijua. 2Wewe unajua nikaapo na niinukapo; unayajua mawazo yangu tokea mbali sana. 3Unachunguza wenendo wangu na kulala kwangu; unazijua njia zangu zote. 7Niende wapi mbali na roho yako? Niende wapi niukimbie uwepo wako? 8Kama nikipaa mbinguni, uko huko; kama nikifanya kitanda changu Kuzimuni, tazama, uko huko. 9Kama nikipaa kwa mbawa za asubuhi na kwenda kuishi pande za mwisho wa bahari, 10hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika. 13Wewe uliumba sehemu zangu za ndani; uliniumba tumboni mwa mama yangu. 14Nitakusifu, kwa maana nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu. Nafsi yangu yalijua hili vizuri sana.

Injili

Mt 18:1–5, 10

1Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, “Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?” 2Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao, 3na kusema, “Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu. 4Hivyo yeyote ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni. 5Na yeyote ampokeaye mtoto mdogo kwa jina langu anipokea mimi. 10Tazameni kwamba msije mkamdharau mmoja wa wadogo hawa. Kwa maana nawambieni kuwa mbinguni kuna malaika wao siku zote wakiutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.

Watakatifu wa 2 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki