Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 1 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 1 Oktoba 2026
Alhamisi · Juma la 26 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Alhamisi ya Juma la 26 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Teresia wa Mtoto Yesu, bikira na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
21Iweni na huruma juu yangu mimi, muwe na huruma juu yangu mimi, rafiki zangu, kwa maana mkono wa Mungu umenigusa mimi. 22Kwa nini mnanitesa mimi kama ninyi mlikuwa Mungu? kwa nini hamjatosheka bado kwa kula mwili wangu? 23Laiti, hayo maneno yangu yangekuwa yameandikwa chini! Laiti, hayo yangekuwa yameandikwa katika kitabu! 24Laiti, kwa kalamu ya chuma na risasi hayo yangekuwa yamechorwa katika mwamba siku zote! 25Lakini kama ilivyo kwangu mimi, Mimi ninafahamu kwamba mkombozi wangu anaishi, na kwamba hata mwisho atasimama katika nchi; 26baada ya ngozi yangu, hivyo ndivyo, mwili huu, unaharibiwa, ndipo katika mwili wangu mimi Nitamwona Mungu. 27Mimi nitamwona yeye kwa macho yangu mwenyewe-Mimi, na siyo mtu mwingine. Moyo wangu hushindwa ndani yangu mimi.
Wimbo wa katikati
7Sikia, sauti yangu nikuitapo, Yahwe! Unihurumie, na unijibu! 8Moyo wangu huongea kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Nami nautafuta uso wako, Yahwe! 9Usiufiche uso wako mbali na mimi; usinikasirikie mimi mtumishi wako! Wewe umekuwa msaada wangu; usiniache wala kunitelekeza, Mungu wa wokovu wangu! 13Kitu gani kingeweza kunitokea kama nisingeamini kuwa nitauona uzuri wa Yahwe katika nchi ya walio hai? 14Umngoje Yahwe; uwe imara, na moyo wako uwe jasiri! Umngoje Yahwe!
Injili
1Baada ya mambo hayo, Bwana akachagua sabini wengine, na kuwatuma wawili wawili wamtangulie katika kila mji na eneo alilotarajia kwenda. 2Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache. Hivyo basi muombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume haraka wafanyakazi katika mavuno yake. 3Enendeni katika miji. Angalieni, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. 4Msibebe mfuko wa pesa, wala mikoba ya wasafiri, wala viatu, wala msimsalimie yeyote njiani. 5Katika nyumba yeyote mtakayo ingia, kwanza semeni, 'Amani iwe katika nyumba hii.' 6kama mtu wa amani yupo pale, amani yenu itabaki juu yake, lakini kama sivyo, itarudi kwenu. 7Bakini katika nyumba hiyo, kuleni na mnywe watakachokitoa, kwa maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msihame kutoka nyumba hii kwenda nyingine. 8Mji wowote muuingiao, na wakawapokea, kuleni chochote kitakachowekwa mbele yenu, 9na ponyeni wagonjwa waliomo humo. Semeni kwao, 'Ufalme wa Mungu umekuja karibu yanu' 10Lakini katika mji wowote mtakaoingia, na wasiwapokee, nendeni nje katika barabara na semeni, 11'Hata vumbi katika mji wenu lililonata miguu mwetu tunalikung'uta dhidi yenu! Lakini tambueni hili, Ufalme wa Mungu umekaribia.' 12Ninawambieni kwamba siku ya hukumu itakuwa ni usitahamilivu zaidi kwa Sodoma kuliko mji huo.
Watakatifu wa siku
- Mt. Teresia wa Mtoto Yesu, bikira na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki