Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 3 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Oktoba 2026

Jumamosi · Juma la 26 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 26 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ayu 42:1–3, 5–6, 12–17

1Kisha Ayubu akamjibu Yahweh na kusema, 2“Ninajua kwamba unaweza kufanya mambo yote, ya kuwa hakuna kusudi lako linaweza kuzuiliwa. 3Ni nani huyo ambaye pasipo maarifa huificha mipango? Kwa kweli nilisema mambo ambayo sikuyaelewa, mambo magumu kwangu kuyafahamu, ambayo juu yake sikujua chochote. 5Nimekuwa nikikusikia kwa usikivu wa sikio langu, lakini sasa jicho langu linakuona wewe. 6Basi ninajidharau mwenyewe; ninatubu kwa mavumbi na majivu.” 12Yahweh aliubarikiwa mwisho wa maisha ya Ayubu kuliko mwanzo wake; alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, ngamia elfu sita, jozi elfu moja, na punda jike elfu moja. 13Pia alikuwa na wana saba na mabinti watatu. 14Binti wa kwanza alimwita Yemima, na wa pili Kezia, na wa tatu Kerenihapuki. 15Katika nchi yote hawakupatikana wanawake wazuri kama mabinti wa Ayubu. Baba yao aliwapa urithi miongoni mwa kaka zao. 16Baada ya haya, Ayubu aliishi miaka 140; aliwaona wana wake na wana wa wanawe, hata kizazi cha nne. 17Basi Ayubu alifariki, akiwa mzee na akijawa na siku nyingi.

Wimbo wa katikati

Zab 119:66, 71, 75, 91, 125, 130

66Unifundishe utambuzi sahihi na uelewa, kwa kuwa nimeamini katika amri zako. 71Ni vizuri kwangu kuwa nimeteseka ili niweze kujifunza sheria zako. 75Ninajua, Yahwe, kuwa amri zako ni za haki, na kuwa katika uaminifu ulinitesa. 91Vitu yote yaliendelea mpaka leo hii, kama vile ulivyosema katika amri zako za haki, maana vitu vyote ni watumishi wako. 125Mimi ni mtumishi wako; unipe uelewa ili niweze kuzijua amri za agano lako. 130Ufafanuzi wa maneno yako huleta nuru; na kumpa ufahamu mjinga.

Injili

Lk 10:17–24

17Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, “Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako.” 18Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi. 19Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru. 20Hata hivyo msifurahi tu katika hili, kwamba roho zinawatii, lakini furahini zaidi kwamba majina yenu yameandikwa mbinguni.” 21Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako.” 22“Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake.” 23Akawageukia wanafunzi, akasema faraghani, “Wamebarikiwa wayaonayo haya ambayo ninyi mnayaona. 24Ninawambia ninyi, kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mambo myaonayo, na hawakuyaona, na kusikia kusikia mnayoyaikia, na hawakuyasikia.”

Watakatifu wa 3 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki