Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sulemani

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sulemani

BWANA amtokea Sulemani tena

1 Fal 9:1–9 · 2 Nya 7:11–22

1 Wafalme

1 Fal 9:1–9

1Sulemani alipomaliza kulijenga hekalu la BWANA, na ikulu ya mfalme, na baada ya kukamilisha vyote alivyokusudia kufanya,

2BWANA alionekana kwa Sulemani kwa mara ya pili, kama alivyoonekana kwake kule Gibeoni.

3Na BWANA akamwambia, “ Nimeyasikia maombi yako na dua zako ambazo umeniomba. Nimeitakasa nyumba hii ambayo umeijenga, kwa ajili yangu, ili niweke jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu yatakuwa humo kwa nyakati zote.

4Lakini pia na wewe, kama utatembea mbele zangu kama Daudi baba yako alivyotembea kwa haki na unyofu katika moyo wako, ukitii yote niliyokuamuru na kuyashika maagizo na sheria zangu,

5ndipo nitakapoimarisha kiti cha enzi kwa Israeli milele, kama nilivyomwahidi baba yako Daudi, nikiseama, 'uzao wako hautaondoka katika kiti cha enzi cha Israeli.

6Lakini kama utageuka, wewe au watoto wako, na kutozishika amri zangu na maagizo yangu ambayo nimeyaweka mbele zako, na kama utaenda kuabudu miungu mingine na kuisujidia,

7basi nitaikatilia mbali Israeli kutoka katika ardhi niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli itakuwa mfano wa kukejeliwa na kitu cha kutusiwa katika mataifa yote.

8Ijapokuwa hekalu hili limetukuka sasa, kila mtu atakayepita pembeni yake atasituka na kuzoomea. Watajiuliza, 'Kwa nini BWANA amefanya hili katika chi hii na kwa nyumba hii?'

9Na wengine watajibu, 'Ni kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wao, ambaye aliwaleta mababu zao toka Misri, na sasa wamegeukia miungu mingine ambayo wameiinamia na kuisujudu. Hiyo ndiyo sababu BWANA amewaletea majanga haya yote.”

2 Mambo ya Nyakati

2 Nya 7:11–22

11Hivyo Selemani akaimaliza nyumba ya Yahwe na nyumba yake mwenyewe. Kila kitu kilichokuja katika moyo wa Selemani kwa ajili ya kukitengeneza katika nyumba ya mfalme na katika nyumba yake mwenyewe, alikitimiza kwa mafanikio.

12Yahwe akamtokea Selemani usiku na kusema kwake, “Nimesikia maombi yako, na nimeichagua sehemu hii kwa ajili yangu mwenyewe kama nyumba ya dhabihu.

13Kama nitazifunga mbingu ili kwamba kusiwepo mvua, au kama nitaamuru nzige waimeze nchi, au kama nitatuma magonjwa kati kati ya watu wangu,

14kisha watu wangu, ambao wameitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, kuomba, kuutafuta uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya, nitasikia kutoka mbinguni, kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.

15Sasa macho yangu yatakuwa wazi na masikio yangu yatasikiliza maombi yanayofanywa katika sehemu hii.

16Kwa maana sasa nimeichagua na kauitakasa nyumba hii ili kwamba jina langu lipate kuwa humo milele. Masikio yangu na moyo wangu vitakuwako kila siku.

17Kwako wewe, kama utatembe mbele zangu kama baba yako Daudi alivyotembea, ukitii yote nilyokuamuru na kuzishika sheria zangu na maagizo yangu,

18basi nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyosema katika agano na Daudi baba yako, niliposema, 'Mzaliwa wako hatashindwa kamwe kuwa mtawala katika Israeli.'

19Lakin ukigeuka, na kuzisahau sheria zangu na amri amabzo nimeweka mbele yenu, na kama utaenda kuabudu miungu wengine na kuwasujudia,

20basi nitawang'oa kutoka kwenye nchi yangu amabayo nimewapa. Nyumba hii ambayo nimeitakasa kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali kutoka mbele zangu, na nitaifanya kuwa methali na utani miongini mwa watu wote.

21Ingawa hekalu hili hili zuri sana kwa sasa, kila mtu apitaye karibu yake atashangazwa na ataguna. Watauliza, 'Kwa nini Yahwe ameifanyia hivi nchi hii na nyumba hii',

22wengine watajibu, 'Kwa sababu walimsahau Yahwe, Mungu wao, ambaye alikuwa amewatoa babu zao nje ya nchi ya Misiri, na wakashikamana na miungu wengine na kuwainamia chini na kuwaabudu. Hii ndiyo maana Yahwe ameleta majanga haya yote juu yao”

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY