Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sauli na Daudi

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sauli na Daudi

Ushindi wa Daudi

2 Sam 8:1–14 · 1 Nya 18:1–13

2 Samweli

2 Sam 8:1–14

1ikawa baada ya haya Daudi aliwashambulia Wafilisti na kuwashinda. Hivyo Daudi akaichukua Gathi na vijiji vyake kutoka katika mamlaka ya wafilisti.

2Kisha akaishinda Moabu na akawapima watu wake kwa mstari kwa kuwafanya walale chini juu ya ardhi. Alipima mistari miwili ya kuua, na mstari mmoja kamili kuwahifadhi hai. Hivyo Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakaanza kumlipa kodi.

3Kisha Daudi akamshinda Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, Hadadezeri aliposafiri kuurudisha ufalme wake katika mto Frati.

4Daudi aliteka magari 1,700 ya farasi na askari ishirini elfu waendao kwa miguu. Daudi akawakata miguu farasi wa magari, lakini akahifadhi wakutosha magari mia moja.

5Wakati Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadeziri mfalme wa Soba, Daudi akaua katika Washami watu ishirini na mbili elfu.

6Daudi akaweka ngome huko Shamu ya Dameski, na Washami wakawa watumishi wake na wakaleta kodi. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alikokwenda.

7Daudi akachukua ngao za dhahabu walizokuwa nazo watumishi wa Hadadezeri naye akazileta Yerusalemu.

8Mfalme Daudi akachukua shaba nyingi kutoka Beta na Berosai, miji ya Hadadezeri.

9Wakati Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri,

10Tou akamtuma Hadoramu mwanawe kwa mfalme Daudi kumpa salamu na kumbariki, kwa kuwa Daudi alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda, maana Hadadezeri alikuwa amepiga vita dhidi ya Tou. Hadoramu akaja pamoja na vitu vya fedha, dhahabu, na shaba.

11Mfalme Daudi akaviweka wakfu vitu hivi kwa ajili ya Yahwe, pamoja na fedha na dhahabu kutoka katika mataifa yote aliyokuwa ameyashinda-

12kutoka Shamu, Moabu, Waamoni, Wafilist, Waamaleki, pamoja na nyara zote alizoziteka kutoka kwa Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.

13Jina la Daudi likajulikana sana alipowashinda washami katika bonde la Chumvi, pamoja na watu wao wapatao elfu kumi na nane.

14Akaweka ngome katika Edomu yote, na Waedomu wote wakawa watumishi wake. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.

1 Mambo ya Nyakati

1 Nya 18:1–13

1Baada ya haya Daudi akawashambulia Wafilisti na kuwashinda. Alichukuwa Gathi na vijiji vyake katika utawala wa Wafilisti.

2Kisha akamshinda Moabu, na Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakamlipa ushuru maalumu.

3Daudi kisha akamshinda Hadadezeri, mfalme wa Zoba huko Hamathi, wakati Hadadezeri alipo kuwa akisafiri kuimarisha utawala wake kwa Mto wa Frati.

4Daudi akateka magari ya farasi elfu, wanaume wa farasi elfu saba, na wanajeshi wa miguu elfu ishirini. Daudi aliwajeruhi farasi wote wagari, lakini akahifadhi baadhi kwa ajili ya magari ya farasi mia moja.

5Waaramia wa Damasko walipo kuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Zoba, Daudi aliua wanaume elfu ishirini na mbili wa Kiaramia.

6Kisha Daudi akaweka vikosi huko Aramu ya Damasko, na Waaramia wakawa watumishi wake na wakamletea ushuru maalaumu. Yahweh alimpatia Daudi ushindi popote alipoenda.

7Daudi alichukua ngao za dhahabu zilizo kuwa kwa watumishi wa Hadadezeri na kuleta Yerusalemu.

8Kutoka Tibhathi na Kuni, miji ya Hadadezeri, Daudi alichukuwa shaba nyingi sana. Ilikuwa shaba hii ambayo baadae Sulemani alifanya saani ya shaba, nguzo, na vifaa vya shaba.

9Wakati Toi, mfalme wa Hamathi, alipo sikia kuwa Daudi ameshinda majeshi yote ya Hadadezeri mfalme wa Zoba,

10Toi akamtuma Hadoramu mwanae kwa Mfalme Daudi kumsalimia na kumbariki, kwasababu Daudi amepigana na Hadadezeri na kumshinda, na kwasababu Hadadezeri alifanya vita na Toi. Hadoramu alipeleka vifaa vya fedha, dhahabu, na shaba.

11Mfalme Daudi alivitenga hivi vitu kwa ajili ya Yahweh, pamoja na fedha na dhahabu aliyo ibeba kutoka kwa mataifa yote: Edomu, Moabu, watu wa Amoni, Wafilisti, na Waamaleki.

12Abishai mwana wa Zeruia akawaua Waedomi elfu kumi na nane katika Bonde la Chumvi.

13Alieka vikosi huko Edomu, na Waedomi wote wakawa watumishi wa Daudi. Yahweh alimpa Daudi ushindi pote alipoenda.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY