Bible Explorer

Gundua › Injili kando kwa kando › Mafundisho

Injili kando kwa kando · Mafundisho

Maelezo ya mfano wa mpanzi

Mt 13:18–23 · Mk 4:13–20 · Lk 8:11–15

Mathayo

Mt 13:18–23

18. Sasa sikilizeni mfano wa mpanzi.

19Wakati yeyote asikiapo neno la ufalme na asilifahamu, ndipo mwovu huja na kukinyakua kilichokwisha kupandwa ndani ya moyo wake. Hii ni mbegu ile iliyopandwa kando ya njia.

20Yeye aliyepandwa katika miamba ni yule asikiaye neno na kulipokea haraka kwa furaha.

21Bado hana mizizi ndani yake, ila huvumilia kwa kitambo kifupi. Wakati matatizo au mateso yanapotokea kwa sababu ya neno hujikwaa ghafla.

22Aliyepandwa kati ya miti ya miiba, huyu ni yule alisikiaye neno lakini masumbuko ya ulimwengu na udaganyifu wa utajiri hulisonga lile neno lisije likazaa matunda.

23Aliyepandwa kwenye udongo mzuri, huyu ni yule asikiaye neno na kulifahamu. Huyu ni yule azaaye matunda na kuendelea kuzaa moja zaidi ya mara mia, nyingine sitini, nyingine thelathini.''

Marko

Mk 4:13–20

13Na akasema kwao, “Je hamuelewi mfano huu? Mtawezaje kuelewa mifano mingine?.

14Mpanzi alipanda neno.

15Baadhi ni wale walioanguka pembeni mwa njia, mahali neno lilipopandwa. Na walipolisikia, mara Shetani akaja na kulichukua neno ambalo lilipandwa ndani yao.

16Na baadhi ni wale waliopandwa juu ya mwamba, ambao, wanapolisikia neno, kwa haraka wanalipokea kwa furaha.

17Na hawana mizizi yoyote ndani yao, lakini huvumilia kwa muda mfupi. Halafu tabu na masumbufu vinapokuja kwa sababu ya neno, mara hujikwaa.

18Na wengine ni wale waliopandwa katika miiba. Wanalisikia neno,

19lakini masumbufu ya dunia, udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine, huwaingia na kulisonga neno, na linashindwa kuzaa matunda.

20Kisha kuna wale ambao wamepandwa kwenye udongo mzuri. Wanalisikia neno na kulipokea na huzaa matunda: baadhi thelathini, na baadhi sitini, na baadhi mia moja.”

Luka

Lk 8:11–15

11Na hii ndiyo maana ya mfano huu. Mbegu ni neno la Mungu.

12Mbegu zile zilizoanguka kando kando ya njia ndiyo wale watu wanaolisikia neno, na baadaye mwovu shetani hulichukua mbali kutoka moyoni, ili kwamba wasiamini na kuokolewa.

13Kisha na zile zilizoangukia kwenye mwamba ni watu wale wanaosikia neno na kulipokea kwa furaha lakini hawana mizizi yeyote, wanaamini tu kwa muda mfupi, na wakati wa majaribu huanguka.

14Na mbegu zile zilizoangukia kwenye miiba ni watu wanaosikia neno, lakini wanapoendelea kukua husongwa na huduma na utajiri na ubora wa maisha haya na hawazai matunda.

15Lakini zile mbegu zilizoangukia kwenye udongo mzuri ni wale watu, ambao ni wanyeyekevu na mioyo mizuri, baada ya kulisikia neno hulishikilia na likawa salama na kuazaa matunda ya uvumilivu.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY