2na Yohana akiwa gereszani aliposikia akiwa juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake,
3na wakamuuliza, “Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?”
4Yesu akajibu na kusema kwao “Nendeni mkamtaarifu Yohana yale mnayoyaona na yale mnayoyasikia.
5Watu wasioona wanapata kuona, viwete wanatembea, wakoma wanatakaswa, watu wasiosikia wanasikia tena, watu waliokufa wanafufuliwa kupata uhai, na watu wahitaji wanahubiriwa habari njema.
6Na amebarikiwa yule asiyeona shaka juu yangu.
7Pindi watu hawa walipoondoka, Yesu alianza kusema na umati juu ya Yohana, “Ni nini mlikwenda kuona katika jangwa—tete likitikiswa na upepo?
8Lakini nini mlikwenda kuona—mtu aliyevaa mavazi mololo? Hakika, wale wavaao mavazi mololo hukaa katika nyumba za wafalme.
9Lakini mliondoka kuona nini-Nabii? Ndiyo, nawaambia, na zaidi ya Nabii.
10Huyu ndiye aliyeandikiwa, 'Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, ambaye ataandaa njia yako mbele yako.
11Mimi nawaambia kweli, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkubwa kuliko yeye.
12Toka siku za Yohana Mbatizaji mpaka sasa, ufalme wa Mbinguni ni wa nguvu, na watu wenye nguvu, huuchukua kwa nguvu.
13Kwa kuwa manabii na sheria, ikamelcuwa wakitabiri mpaka kwa Yohana.
14Na kamamko tayari kukubali, huyu ni Eliya, yule ajaye.
15Aliye na masikio ya kusikia na asikie.
16Nikilinganishe na nini kizazi hiki? Ni mfano wa watoto wanaocheza maeneo ya sokoni, wanaokaa na kuitana
17na kusema, 'Tuliwapigia zomari na hamkucheza. Tuliomboleza, na hamukulia.'
18Kwa kuwa Yohana alikuja bila kula mkate au kunywa mvinyo, na wakawa wanasema, 'Ana pepo.'
19Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema 'Angalia, ni mtu mlaji na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!' Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.''