Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › Waebrania 10:25

Mstari wa Biblia · ULB

Waebrania 10:25

Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia.

Soma sura nzima: Waebrania 10

Katika muktadha

22na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi.

23Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu.

24Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema.

25Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia.

26Kama tukifanya makusudi kuendelea kutenda dhambi baada ya kuwa tumepokea elimu ya ukweli, Dhabihu nyingine ya dhambi haisalii tena.

27Badala yake, kuna tarajio pekee la hukumu ya kutisha, na ukali wa moto ambao utawateketeza maadui wa Mungu.

28Yeyote ambaye ameikataa sheria ya Musa hufa bila rehema mbele ya ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.

Waebrania 10

Kwa Kiingereza

Berean Standard BibleHebrews 10:25Let us not neglect meeting together, as some have made a habit, but let us encourage one another, and all the more as you see the Day approaching.

Marejeo mtambuka

Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.

Mdo 2:42Wakaendelea katika mafundisho ya mitume na ushirikiano, katika kuumega mkate na katika maombi.
1 The 5:11Kwa hiyo, farijianeni na kujengana ninyi kwa ninyi, kama ambavyo tayari mnafanya.
Mt 18:20Kwa kuwa wawili au watatu wakikusanyika pamoja kwa jina langu, Mimi niko katikati yao.
Ebr 3:13Badala yake, mhamasishane kila siku kila mmoja na mwenzie, ili kila iitwapo leo mtamani, ili kwamba mmoja kati yenu asifanywe kuwa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
1 Kor 5:4Mnapokutanika pamoja katika jina la Bwana wetu Yesu, na roho yangu ipo pale kama kwa nguvu za Bwana wetu Yesu, nimekwisha mhukumu mtu huyu.
1 The 4:18Kwa hiyo, mfarijiane ninyi kwa ninyi kwa maneno haya.
Mdo 20:7Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekusanyika pamoja ili kuumega mkate, Paulo alizungumza na Waamini. Alikuwa akipanga kuondoka kesho yake, hivyo akaendelea kuongea hadi usiku wa manane.

Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki