Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 27 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 27 Desemba 2027
Jumatatu · Kipindi cha Noeli
Sikukuu na watakatifu
Mt. Yohane, mtume na mwinjili
Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Kile kilichokuwapo tangu mwanzo-kile tulichokisikia, kile tulichokiona kwa macho yetu, kile tulichokitazama, na mikono yetu imekishika-kuhusu Neno la uzima. 2Na ule uzima ulifanywa kujulikana wazi, na tumeuona, na kuushuhudia, na kuwatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa kwa Baba na ulifanywa kujulikana kwetu. 3Kile tulichokiona na kukisikia twakitangaza kwenu pia, ili kwamba muweze kujumuika pamoja nasi, na ushirika wetu pamoja na Baba na Mwanae Yesu Kristo. 4Na tunawandikia mambo haya ninyi ili kwamba furaha yetu iwe timilifu.
Wimbo wa katikati
1Yahwe anatawala; nchi ishangilie; visiwa vingi na vifurahi. 2Mawingu na giza vyamzunguka. Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake. 5Milima huyeyuka kama nta mbele za Yahwe, Bwana wa dunia yote. 6Mbingu hutangaza haki yake, na mataifa yote huuona utukufu wake. 11Nuru imepandwa kwa ajili ya wenye haki na furaha kwa ajili ya wanyoofu wa moyo. 12Furahini katika Yahwe, enyi wenye haki; na mpeni shukurani mkumbukapo utakatifu wake.
Injili
2Kwa hiyo akakimbia mbio kwenda kwa Simon Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, kisha akawaambia, “wamemchukua Bwana kaburini, nasi hatujui kule walikomlaza.” 3Kisha Petro na yule mwanafunzi mwingine wakatoka, kuelekea kaburini. 4Wote walipiga mbio kwa pamoja; yule mwanafunzi mwingine alikimbia kwa kasi zaidi ya Petro nakufika kaburini wa kwanza. 5Akasimama na kisha kuangalia kaburini; akaiona ile sanda ya kitani imelala, lakini hakuingia ndani. 6Kisha Simon Petro naye akafika akaingia ndani ya Kaburi. Akaiona ile sanda ya kitani imelala pale 7na ile leso iliyokuwa kichwani pake haikuwa imelala pamoja na zile sanda za kitani bali ilikuwa imelala pembeni peke yake. 8Ndipo yule mwanafunzi mwingine naye alipoingia ndani ya kaburi; akaona na kuamini.
Watakatifu wa siku
- Mt. Yohane, mtume na mwinjili
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili C, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki