Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 10 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 27 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 10 Desemba 2027
Ijumaa · Wiki ya 25 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Ishara ya Mama Mtakatifu Sana wa Mungu iliyotokea Novgorod Kuu (1170)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
6Sasa tunawaagiza, ndugu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, kwamba mwepuke kila ndugu ambaye anaishi maisha ya uvivu na siyo kwa kutokana na desturi ambazo mlipokea kutoka kwetu. 7Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ni sawa kwenu kutuiga sisi. Hatukuishi miongoni mwenu kama wale ambao hawakuwa na nidhamu. 8Na hatukula chakula cha mtu yeyote bila kukilipia. Badala yake, tulifanya kazi usiku na mchana kwa kazi ngumu na kwa shida, ili tusiweze kuwa mzigo kwa yeyote katika ninyi. 9Tulifanya hivi si kwa sababu hatuna mamlaka. Badala yake, tulifanya hivi ili tuwe mfano kwenu, ili kwamba mweze kutuiga sisi. 10Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, “Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile.” 11Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu. 12Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe. 13Lakini ninyi, ndugu, msizimie roho katika kufanya yaliyo sahihi. 14Ikiwa mtu yeyote hataki kutii neno letu katika waraka huu, mwe makini naye na msiwe na ushirika pamoja naye, ili kwamba aweze kuaibika. 15Msimchukulie kama adui, lakini mwonyeni kama ndugu. 16Bwana wa amani mwenyewe awape amani wakati wowote katika njia zote. Bwana awe nanyi nyote. 17Hii ni salam yangu, Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe, ambayo ni alama katika kila waraka. Hivi ndivyo niandikavyo. 18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iweze kuwa nanyi nyote.
Injili
12Hivyo akawaambia, 'Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi. 13Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, 'fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.' 14Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, 'Hatutaki mtu huyu atutawale.' 15Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara. 16Wa kwanza akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi. ' 17Huyo Ofisa akamwambia, Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi. ' 18Wa pili akaja, akasema, 'Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.' 19Huyo Afisa akamwambia, 'Chukua mamlaka juu ya miji mitano.' 20Na mwingine akaja, akasema, 'Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa, 21kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda. ' 22Huyo Ofisa akamwambia, 'Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda. 23Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida? 24Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, 'Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.' 25Wakamwambia, 'Bwana, yeye ana mafungu kumi. ' 26'Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa. 27Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu. '' 28Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Mkuu Yakobo Mwajemi (421)
- Mtakatifu Mtawa Paladio wa Aleksandria (karne ya 6-7)
- Mtakatifu Mtawa Romano, mtenda miujiza (karne ya 5)
- Kupatikana kwa masalia ya Mwana wa Mfalme Mwaminifu Vsevolod wa Novgorod, aliyeitwa Gabrieli katika Ubatizo mtakatifu, mtenda miujiza wa Pskov (1192)
- Askofu Mtakatifu Yakobo, Askofu wa Rostov (1392)
- Mbarikiwa Andrea wa Simbirsk (1841)
- Wafiadini wa Kikasisi Nikolao, Askofu Mkuu wa Vladimir, Basili, Boris, Theodoro, Nikolao, Aleksi, Yohana, Sergio, Yohana, Sergio, Nikolao, Demetrio, Vladimir, Yohana, mapadri, Watawa Wafiadini Yoasafu, Kronido, Nikolao, Ksenofoni, Aleksi, Apolo, Serafim, Nikoni na Mfiadini Yohana (1937)
- Watawa Wafiadini 17 huko India (karne ya 4)
- Ikoni za Mama wa Mungu “Ishara”: ya Kursk ya Mzizi (1295), ya Abalak (1637), ya Tsarskoye Selo, ya Verkhny Tagil (1753), ile iitwayo “Ya Nyumba ya Wageni” (karne ya 18), ya Serafim-Ponetayevka (1879)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 27 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 10 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki