Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 9 Desemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 26 Novemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 9 Desemba 2027
Alhamisi · Wiki ya 25 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Alipio, mkaa nguzoni (640)
Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
13Lakini inatupasa tumshukuru Mungu kila mara kwa ajili yenu ndugu mpendwao na Bwana. Kwa sababu Bwana aliwachagua ninyi kama malimbuko ya wokovu kwa utakaso wa Roho na imani katika ile kweli. 14Hiki ndicho alichowaitieni ninyi, kwamba kupitia injili muweza kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. 15Kwa hiyo, ndugu, simameni imara. Ueleweni ule utamaduni mliofundishwa, kwa neno au kwa barua yetu. 16Sasa, Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu aliyetupenda na kutupa faraja ya milele na ujasiri mwema kwa ajili ya maisha yajayo kupitia neema, 17awafariji na kuifanya imara mioyo yenu katika kila neno na kazi njema. 3:1Na sasa, ndugu, tuombeeni, kwamba neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa, kama ilivyo pia kwenu. 2Ombeni kwamba tuweze kuokolewa kutoka katika uovu na watu waasi, kwa kuwa si wote wana imani. 3Lakini Bwana ni mwaminifu, ambaye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu. 4Tunaujasiri katika Bwana kwa ajili yenu, kwamba mnatenda na mtaendelea kutenda mambo ambayo tunawaagiza. 5Bwana aweze kuongoza mioyo yenu katika upendo na katika uvumilivu wa Kristo.
Injili
31Baada ya kuwakusanya wale kumi na wawibili, akawaambia, 'Tazama, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote ambayo yameandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Adamu yatakamilishwa. 32Kwa maana atatiwa mikononi mwa watu wa Mataifa na atatendewa dhihaka na jeuri, na kutemewa mate. 33Baada ya kumchapa viboko watamwua na siku ya tatu atafufuka. ' 34Hawakuelewa mambo haya, na neno hili lilikuwa limefichwa kwao, na hawakuelewa mambo yaliyosemwa.
Watakatifu wa siku
- Kuwekwa wakfu kwa kanisa la Mfiadini Mkuu Georgi huko Kyiv (1051-1054)
- Askofu Mtakatifu Inokenti, Askofu wa Irkutsk (1731)
- Wafiadini wa Kikasisi Nikolao, Yohana, Georgi, Nazario, Basili, Basili, Eliya, Basili, Danieli, Mikaeli, Nikolao, mapadri, Mtawa Mfiadini Tikhon (1937)
- Mfiadini Petro (baada ya 1937)
- Mtakatifu Mtawa Yakobo, mkaa jangwani wa Shamu (457)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 26 Novemba katika kalenda ya kanisa ni 9 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki