Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 9 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 9 Desemba 2027
Alhamisi · Juma la 2 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
Alhamisi ya Juma la 2 la Majilio
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: zambarau
Mt. Yohane Diego · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
13Maana mimi Yahwe Mungu wako, nitawashika mkono wako wa kiume, nikikuambia wewe, 'Usiogope; Nitakusaidia wewe. 14Usiogope, Yakobo wewe mdudu, na enyi watu wa Israeli; Nitawasaidia''- hili ni tamko la Yahwe, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli. 15Tazama, ninakufanya wewe kuwa chombo kikali cha kuparulia chenye makali pande mbili; utaparua milima na kuiponda; utafanya vilima kama makapi. 16Utawatawanya wao, na upepo utawabeba na kuwapeka mbali; upepo utawatanya wao. Utashanglia katika Yahwe, utashangiliakatika mtakatifu wa Israeli 17Waliodhulumiwa na masikini wanatafuta maji, lakini hakuna kitu, ndimi zao zimekauka kwa kiu; Mimi Yahwe, nitajibu maombi yao; Mimi Mungu wa Israeli, sitawacha wao. 18Nitatengeneza mikondo ya maji kushusha chini, na chemichem katikati ya mabonde; nitalifanya jangwa kuwa kisima cha maji, na aridhi kavu kuwa chemichem ya maji. 19Katika jangwa nitapanda mierezi, mshita, mhadisi, na mti wa mizeituni. Nitaotesha mberoshi katika uwazi wa jangwa, pamoja na mbono nitapanda mberoshi kitika jangwa lililowazi. 20Nitayafanya haya ili waweze kuona, kutambua na kuelewa kwa pamoja, kwamba mkono wa Yahwe umetenda haya, kama Mtakatifu wa Israeli aliyeliumba.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya sifa. Ya Daudi. Nitakutukuza wewe, Mungu wangu, Mfalme; nitalihimidi jina lako milele na milele. 9Yahwe ni mwema kwa wote; huruma zake zi juu ya kazi zake zote. 10Vyote ulivyo viumba vitakushukuru wewe, Yahwe; waaminifu wako watakutukuza wewe. 11Waaminifu wako watanena juu ya utukufu wa ufalme wako, na watahubiri juu ya nguvu zako. 12Watayafanya matendo makuu ya Mungu ya julikane na wanadamu na utukufu wa fahari ya ufalme wake. 13Ufalme wako ni wa milele, na mamlaka yako ya dumu kizazi hata kizazi.
Injili
11Mimi nawaambia kweli, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkubwa kuliko yeye. 12Toka siku za Yohana Mbatizaji mpaka sasa, ufalme wa Mbinguni ni wa nguvu, na watu wenye nguvu, huuchukua kwa nguvu. 13Kwa kuwa manabii na sheria, ikamelcuwa wakitabiri mpaka kwa Yohana. 14Na kamamko tayari kukubali, huyu ni Eliya, yule ajaye. 15Aliye na masikio ya kusikia na asikie.
Watakatifu wa siku
- Mt. Yohane Diego
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili C, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki