Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 18 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 18 Novemba 2027

Alhamisi · Juma la 33 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 33 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Kutabarukiwa kwa Basilika za Watakatifu Petro na Paulo, mitume · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 50:1–2, 5–6, 14–15

1Zaburi ya Asafu. Mungu, Mwenye nguvu, Yahwe, amenena naye aliita nchi toka mawio ya jua mpaka machweo yake. 2Tokea Sayuni, Mungu ameangaza, ukamilifu wa uzuri. 5Kwa pamoja kusanyikeni waaminifu wangu kwangu, wale waliofanya nami agano kwa sadaka.” 6Mbingu zitatangaza haki yake, kwa maana Mungu mwenyewe ndiye jaji. Serah 14Mtoleeni Mungu sadaka za shukurani, na mlipe viapo vyenu kwa Aliye Juu. 15Mniite katika siku ya shida; nami nitawaokoa

Injili

Lk 19:41–44

41Yesu alipoukaribia mji aliulilia, 42akisema, laiti ungelijua hata wewe, katika siku hii mambo ambayo yanayokuletea amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako. 43Kwa kuwa siku zinakuja ambapo adui zako watajenga boma karibu na wewe, na kukuzunguka na kukukandamiza kutoka kila upande. 44Watakuangusha chini wewe na watoto wako. Hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu haukutambua wakati Mungu alipokuwa anajaribu kukuokoa'.

Watakatifu wa 18 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki