Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 9 Novemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 27 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 9 Novemba 2027
Jumanne · Wiki ya 21 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Mfiadini Nestori wa Thesalonike (karibu 306)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu, 2kwa waumini na ndugu waaminifu katika Kristo walioko Kolosai. Neema iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu. 7Hii ndiyo injili mliyojifunza kutoka kwa Epafra, mpendwa wetu mtumishi mwenzetu, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu. 8Epafra ameufanya ujulikane kwetu upendo wenu katika Roho. 9Kwa sababu ya upendo huu, tangu siku tuliposikia hivi, hatujaacha kuwaombea. Tumekuwa tukiomba kwamba mtajazwa na maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa kiroho. 10Tumekuwa tukiomba kwamba mtatembea kwa ustahimilivu wa Bwana katika njia zipendezazo. Tumekuwa tukiomba kwamba mtazaa tunda katika kila tendo jema na kwamba mtakua katika maarifa ya Mungu. 11Tunaomba mweze kutiwa nguvu katika kila uwezo kulingana na nguvu za utukufu wake katika uvumilivu na ustahimilivu wote.
Injili
1Ilitokea wakati Yesu alipokuwa anaomba mahali fulani, mmoja wa mwanafunzi wake alimwambia, “Bwana, tufundishe sisi kuomba kama Yohana alivyo wafundisha wanafunzi wake'. 2Yesu akawaambia, Msalipo, semeni, 'Baba, Jina lako litakazwe. Ufalme wako uje. 3Utupe mkate wetu wa kila siku. 4Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe wote waliotukosea. Usituongoze katika majaribu.” 5Yesu akawaambia, “Ni nani kwenu atakuwa na rafiki, ambaye atamuendea usiku, na kumwambia, Rafiki niazime mikate mitatu. 6Kwa sababu rafiki yangu amenijia sasa hivi kutoka safarini, nami sina cha kumuandalia.' 7Na yule aliyeko ndani akamjibu, usinitaabishe, Mlango umekwisha kufungwa, na watoto wangu, pamoja nami tumekwisha kulala kitandani. Siwezi kuamka na kukupa wewe mikate. 8Nawaambia, japo kuwa haamki na kukupatia mikate kama rafiki yake, kwa sababu ya kuendelea kumgongea bila aibu, ataamka na kukupatia vipande vingi vya mikate kulingana na mahitaji yako. 9Nami pia nawaambieni, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata, pigeni hodi nanyi mtafunguliwa. 10Kwa kuwa kila mtu aombaye atapokea, na kila mtu atafutaye atapata, na kila mtu apigaye hodi, mlango utafunguliwa kwake.
Watakatifu wa siku
- Wafiadini Kapitolina na Erotiida (304)
- Mtakatifu Mtawa Nestori, mwandishi wa historia, wa Mapango ya Kyiv (karibu 1114)
- Mtakatifu Mtawa Nestori, asiye na elimu ya vitabu, wa Mapango ya Kyiv (karne ya 14)
- Kupatikana kwa masalia ya Mwana wa Mfalme Mwaminifu Andrea wa Smolensk huko Pereslavl-Zalessky (1539)
- Mfiadini Marko na wale walio pamoja naye
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 27 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 9 Novemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki