Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 8 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 8 Novemba 2027

Jumatatu · Juma la 32 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatatu ya Juma la 32 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 139:1–10

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya daudi. Ee Yahwe, wewe umenichunguza, na unanijua. 2Wewe unajua nikaapo na niinukapo; unayajua mawazo yangu tokea mbali sana. 3Unachunguza wenendo wangu na kulala kwangu; unazijua njia zangu zote. 4Kabla hakujawa na neno kwenye ulimi wangu, wewe unalijua kabisa, Yahwe. 5Nyuma yangu na mbele yangu unanizunguka na kuniwekea mkono wako. 6Maarifa hayo ni mengi yananizidi mimi; yako juu sana, nami siwezi kuyafikia. 7Niende wapi mbali na roho yako? Niende wapi niukimbie uwepo wako? 8Kama nikipaa mbinguni, uko huko; kama nikifanya kitanda changu Kuzimuni, tazama, uko huko. 9Kama nikipaa kwa mbawa za asubuhi na kwenda kuishi pande za mwisho wa bahari, 10hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika.

Injili

Lk 17:1–6

1Yesu akawaambia wanafunzi wake, “mambo yasababishayo watu watende dhambi hayana budi kutokea, Lakini ole wake mtu anayeyasababisha! 2Ingekua ni heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito la kusagia shingoni na kutubwa baharini, kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi. 3Jilindeni. Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu msamehe. 4Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, 'ninatubu,' msamehe!” 5Mitume wake wakamwambia Bwana, “tuongezee imani yetu.” 6Bwana akasema, “kama mgekuwa na imani kama punje ya haradarii, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, 'n'goka na ukaote baharini,' nao ungewatii.

Watakatifu wa 8 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki