Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 29 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 29 Oktoba 2027

Ijumaa · Juma la 30 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 30 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Rum 9:1–5

1Nasema ukweli katika Kristo. Sisemi uongo, na dhamira yangu hushuhudia pamoja nami katika Roho Mtakatifu, 2kwamba kuna huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma ndani ya moyo wangu. 3Kwamba ningetamani mimi mwenyewe kulaaniwa na kutengwa mbali na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, wale wa jamii yangu katika mwili. 4Wao ni Waisraeli. Walio na hali ya kufanyika watoto, wa utukufu, wa maagano, na zawadi ya sheria, kumwabudu Mungu, na ahadi. 5Wao ni watangulizi ambako Kristo amekuja kwa heshima kuvaa mwili huu - ambaye yeye ni Mungu wa vyote. Naye asifiwe milele. Amina.

Wimbo wa katikati

Zab 147:12–15, 19–20

12Msifuni Yahwe, Yerusalemu, msifuni Mungu wenu, Sayuni. 13Maana yeye huyakaza mapingo ya malango yako, huwabariki watoto wako kati yako. 14Huletamafanikio ndani ya mipaka yako, hukutosheleza kwa ngano bora. 15Huipeleka amri yake juu ya nchi, amri zake hupiga mbio sana. 19Hutangaza neno lake kwa Yakobo, amri zake na hukumu zake kwa Israeli. 20Hajafanya hivyo kwa taifa linginelo lolote, na kama ilivyo amri zake, hawazijui. Msifuni Yahwe.

Injili

Lk 14:1–6

1Iltokea siku ya Sabato, alipokua akienda nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo kula mkate, nao walikuwa wakimchunguza kwa karibu. 2Tazama, pale mbele yake alikuwa mtu ambaye anasumbuliwa na uvimbe. 3Yesu aliuliza wataalam katika sheria ya Wayahudi na Mafarisayo, “Je, ni halali kumponya siku ya Sabato, au sivyo?” 4Lakini wao walikuwa kimya, kwahiyo Yesu akamshika, akamponya na kumruhusu aende zake. 5Naye akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye ana mtoto au ng'ombe anatumbukia kisimani siku ya Sabato hata mvuta nje mara moja?” 6Wao hawakuwa na uwezo wa kutoa jibu kwa mambo haya.

Watakatifu wa 29 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki