Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 26 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 26 Oktoba 2027

Jumanne · Juma la 30 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 30 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Rum 8:18–25

18Kwa kuwa nayahesabu mateso ya wakati huu kuwa si kitu nikilinganisha na utukufu utakaofunuliwa kwetu. 19Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. 20Kwa maana uumbaji pia ulitiishwa chini ya ubatili, si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha. Ni katika tumaini 21kwamba uumbaji wenyewe nao utawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, na kuingizwa katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. 22Kwa maana twajua ya kuwa uumbaji nao pia unaugua na kuteseka kwa uchungu pamoja hata sasa. 23Si hivyo tu, ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho - sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukisubiri kufanywa wana, yaani ukombozi wa miili yetu. 24Kwa maana ni kwa taraja hili tuliokolewa. Lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana hakuna taraja tena, kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho? 25Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.

Wimbo wa katikati

Zab 126:1–6

1Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Bwana alipowarejesha mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto. 2Vinywa vyetu vilijawa na vicheko na ndimi zetu zilijawa na kuimba. Kisha wakasema kati ya mataifa, “Yahwe amewatendea mambo makuu.” 3Yahwe alitufanyia mambo makuu; ni furaha gani tuliyokuwa nayo! 4Ee Yahwe, uwarejeshe mateka wetu, kama vijito vya kusini. 5Wale wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha. 6Yeye aendaye akilia, akibeba mbegu kwa ajili a kupanda, atarudi tena kwa kelele za furaha, akileta miganda yake.

Injili

Lk 13:18–21

18Yesu akasema, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini, na naweza kuulinganisha na nini? 19Ni kama mbegu ya haradari aliyoitwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake, na ikamea ikawa mti mkubwa, na ndege wa mbinguni wakajenga viota vyao katika matawi yake. 20Tena akasema, “Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? 21Ni kama chachu ambayo mwanamke aliichukua na kuchanganyakwenye vipimo vitatu vya unga hata ukaumuka.”

Watakatifu wa 26 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki