Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 25 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 25 Oktoba 2027

Jumatatu · Juma la 30 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatatu ya Juma la 30 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Rum 8:12–17

12Hivyo basi, ndugu zangu, sisi tu wadeni, lakini si kwa mwili kwamba tuishi kwa jinsi ya mwili. 13Maana ikiwa mnaishi kwa jinsi ya mwili, mpo karibu kufa, lakini ikiwa kwa Roho mnayafisha matendo ya mwili, nanyi mtaishi. 14Maana kama ambavyo wengi wanaongozwa na Roho wa Mungu, hawa ni wana wa Mungu. 15Kwa kuwa hamkupokea roho wa utumwa tena hata muogope. Badala yake, mlipokea roho ya kufanywa kuwa wana, ambayo kwayo tunalia, “Abba, Baba!” 16Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa tu watoto wa Mungu. 17Ikiwa tu watoto, basi tu warithi pia, warithi wa Mungu. Na sisi tu warithi pamoja na Kristo, ikiwa kwa kweli tunateseka na yeye ili tupate kutukuzwa pamoja naye.

Wimbo wa katikati

Zab 68:1, 3, 5–6, 19–20

1Kwa kiongozi wa muziki; Zaburi ya Daudi, wimbo. Mungu ainuke, maadui zake watawanyike; pia wale wamchukiao wakimbie mbele zake. 3Bali wenye haki wafurahi; washangilie mbele za Mungu; washangilie na kufurahi. 5Baba wa yatima, na mwamuzi wa wajane, ni Mungu anayeishi mahali patakatifu. 6Mungu huwaweka wakiwa katika familia; yeye huwafungua wafungwa kwa kuimba bali waasi huishi katika ardhi kavu. 19Abarikiwe Bwana, atubebeaye mizigo yetu, Mungu ambaye ni wokovu wetu. Selah 20Mungu wetu ni Mungu aokoaye; Yahwe Bwana ni yule awezaye kutuokoa sisi dhidi ya kifo.

Injili

Lk 13:10–17

10Sasa Yesu alikuwa akifundisha katika mojawapo ya Masinagogi wakati wa Sabato. 11Tazama, alikuwepo mama mmoja ambaye kwa miaka kumi na minane alikuwa na rohomchafu wa udhaifu, na yeye alikuwa amepinda na hana uwezo kabisa wa kusimama. 12Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umewekwa huru kutoka kwenye udhaifu wako.” 13Akaweka mikono yake juu yake, na mara mwili wake akajinyoosha na akamtukuza Mungu. 14Lakini mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo mtawala akajibu akawambia makutano, “Kuna siku sita ambazo ni lazima kufanya kazi. Njoni kuponywa basi, si katika siku ya Sabato. ' 15Bwana akamjibu na akasema, “wanafiki! Hakuna kila mmoja wenu kufungua punda wako au ng'ombe kutoka zizini na kuwaongoza kumpeleka kunywa siku ya Sabato? 16Hivyo pia binti wa Abrahamu, ambaye Shetani amemfunga kwa miaka kumi na minane, je haikumpasa kifungo chake kisifunguliwe siku ya sabato?” 17Alipokuwa akisema maneno hayo, wale wote waliompinga waliona aibu, bali makutano wote wa wengine walishangilia kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyotenda.

Watakatifu wa 25 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki