Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 25 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 12 Oktoba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 25 Oktoba 2027
Jumatatu · Wiki ya 19 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Wafiadini Probo, Taraka na Androniko (304)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Paulo na Timotheo, watumishi wa Kristo Yesu, Kwa wale walitengwa katika Kristo wanaoishi Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi. 2Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo. 3Namshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbuka ninyi nyote. 4Mara zote katika kila ombi langu kwa ajili yenu ninyi nyote, huwa na furahi ninapowaombea. 5Nina shukrani nyingi kwa sababu ya ushirika wenu katika injili tangu siku ya kwanza mpaka leo. 6Nina hakika kuwa yeye aliyeanzisha kazi njema ndani yenu ataendelea kuikamilisha mpaka siku ya Bwana Yesu Kristo. 7Ni sawa kwangu kujisikia hivi juu yenu ninyi nyote kwa sababu nimewaweka moyoni wangu. Maana ninyi mmekuwa washirika wenza katika neema katika kifungo changu na katika utetezi na uthibitishaji wangu wa injili.
Injili
36Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale. 37Tazama kulikuwa na mwanamke mmoja katika jiji hilo aliyekuwa na dhambi. Akagundua kuwa alikuwa amekaa kwa Farisayo, akaleta chupa ya manukato. 38Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato. 39Na yule farisayo aliyekuwa amemwalika Yesu alipoona hivyo, akawaza mwenyewe akisema, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua huyu ni nani na ni aina gani ya mwanamke anayemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi. 40Yesu akajibu na kumwambia, “Simoni nina kitu cha kukuambia. “Akasema” “Kiseme tu mwalimu!” 41Yesu akasema “Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini. 42Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi? 43Simoni akamjibu na kusema, “Nadhani aliyesamehewa zaidi.”Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.” 44Yesu akamgeukia mwanamke na kusema kwa Simoni, “Unamwona huyu mwanamke. Nimeingia kwenye Nyumba yako. Hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu, lakini huyu, kwa machozi yake, alilowanisha miguu yangu na kuifuta kwa nywele zake. 45Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu. 46Hukuipaka miguu yangu kwa mafuta, lakini ameipaka miguu yangu kwa manukato. 47Kwa jambo hili, nakwambia kwamba alikuwa na dhambi nyingi na amesamehewa zaidi, na pia alipenda zaidi. Lakini aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo tu.” 48Baadaye akamwambia mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa” 49Wale waliokaa mezani pamoja naye wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani mpaka anasamehe dhambi?” 50Na Yesu akamwambia mwanamke, “Imani yako imekuokoa. Enenda kwa amani”
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Kosma, Askofu wa Maiuma, mtunzi wa kanoni (karibu 787)
- Mtakatifu Yohana Mwungamaji (1930)
- Mtawa Mfiadini Laurenti (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, padri (1940)
- Askofu Mtakatifu Nikolao Mwungamaji, Mitropoliti wa Alma-Ata (1955)
- Mfiadini Domnika (286)
- Askofu Mtakatifu Martini Mwenye Huruma, Askofu wa Tours (karibu 400)
- Mtakatifu Mtawa Amfilokio, abati wa Glushitsa (1452)
- Kuhamishwa kutoka Malta hadi Gatchina kwa sehemu ya mti wa Msalaba Utoao Uzima wa Bwana, Ikoni ya Mama wa Mungu ya Philermos na mkono wa kulia wa Mtakatifu Yohana Mbatizaji (1799)
- Ikoni za Mama wa Mungu: ya Yerusalemu (48), ya Yaroslavl ya Smolensk (1642), ya Rudnya (1687) na ya Kaluga (1748)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 12 Oktoba katika kalenda ya kanisa ni 25 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki