Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 9 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 9 Oktoba 2027
Jumamosi · Juma la 27 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 27 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Dionisi, askofu, na wenzake, mashahidi · Kumbukumbu ya hiari
Mt. Yohane Leonardi, padre · Kumbukumbu ya hiari
Mt. Yohane Henry Newman, padre na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
12Naam, mataifa yajihimize yenyewe kuja hadi bonde la Yehoshafati. Kwa maana nitakaa huko kuhukumu mataifa yote ya jirani. 13Wekeni katiki mundu, kwa maana mavuno yameiva. Njoo, muponde zabibu, kwa ajiri pipa la divai limejaa. Vipuri vilivyofurika, kwa sababu uovu wao ni mkubwa sana. 14Kuna mshtuko, mshtuko katika bonde la Hukumu. Kwa maana siku ya Bwana i karibu katika bonde la hukumu. 15Jua na mwezi vinakuwa giza, nyota zimeacha kuangaza. 16Bwana ataunguruma kutoka Sayuni, na kuinua sauti yake kutoka Yerusalemu. Mbingu na nchi zitatikisika, lakini Bwana atakuwa makao kwa ajili ya watu wake, na ngome kwa wana wa Israeli. 17Kwa hiyo mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, anayeishi Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Kisha Yerusalemu itakuwa takatifu, na hakuna jeshi litaklozunguka tena. 18Katika siku hiyo, milima itatayarisha divai nzuri, milima itatiririsha maziwa, miito yote ya Yuda itapita katikati ya maji, na chemchemi zitakuja kutoka nyumba ya Bwana na maji ya bonde la Shitimu. 19Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya vurugu iliyofanyika kwa watu wa Yuda, kwa sababu walimwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao. 20Lakini Yuda utakua mwenyeji milele, na Yerusalemu itakuwa kizazi hata kizazi. 21Nitawalipizia damu yao, ambayo sijajilipizia kisasi, kwa maana Bwana anaishi Sayuni.
Wimbo wa katikati
1Yahwe anatawala; nchi ishangilie; visiwa vingi na vifurahi. 2Mawingu na giza vyamzunguka. Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake. 5Milima huyeyuka kama nta mbele za Yahwe, Bwana wa dunia yote. 6Mbingu hutangaza haki yake, na mataifa yote huuona utukufu wake. 11Nuru imepandwa kwa ajili ya wenye haki na furaha kwa ajili ya wanyoofu wa moyo. 12Furahini katika Yahwe, enyi wenye haki; na mpeni shukurani mkumbukapo utakatifu wake.
Injili
27Ilitokea kwamba alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke fulani alipasa sauti yake zaidi ya wote kwanye mkutano wa watu na kusema “ Limebarikiwa tumbo lililo kuzaa na matiti uliyoyanyonya” 28Lakini yeye akasema, wamebarikiwa wale wasikio neno la Mungu na kulitunza.
Watakatifu wa siku
- Mt. Dionisi, askofu, na wenzake, mashahidi
- Mt. Yohane Leonardi, padre
- Mt. Yohane Henry Newman, padre na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki