Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 25 Septemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 25 Septemba 2027
Jumamosi · Juma la 25 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 25 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Kisha nikainua macho yangu na kuona mtu akiwa na timazi mkononi mwake. 2Nikamwuliza, “Unakwenda wapi?” Akaniambia, “Ninakwenda kuupima Yerusalemu ili kujua upana na urefu wake.” 3Ndipo malaika aliyekuwa anaongea nami akaondoka na malaika mwingine akaenda kukutana naye. 4Malaika wa pili akamwambia, “Nenda uongee na yule kijana umwambie, 'Yerusalemu utakuwa bila kuta kwa sababu ya wingi wa watu na wanyama ndani yake. 5Kwa maana Yahwe asema, Nitakuwa ulinzi wake, na nitakuwa utukufu katikati yake. 10“Imba kwa furaha, binti Sayuni, kwa maana mimi mwenyewe nitakaa nawe! - asema Yahwe 11Mataifa makubwa yataungana na Yahwe siku hiyo. “Nanyi mtakuwa watu wangu; kwa kuwa nitakaa kati yenu,” nanyi mtajua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu.
Wimbo wa katikati
10Sikia neno la Yahwe, mataifa. Litangazeni pembezoni mwa visiwa mbali. Enyi mataifa lazima museme, 'Yule aliyemtawanya Israeli anamkusanya tena na kuwalinda kama mchungaji alindavyo kondoo.' 11Kwa maana Yahwe amemfidia Yakobo na kumkomboa kutoka mkono ambao ulikuwa na nguvu sana kwake. 12Kisha watakuja na kufurahia katika vilele vya Sayuni. Nyuso zao zitamelemeta kwa sababu ya wema wa Yahwe, juu ya nafaka na divai mpya, juu ya mafuta na malimbuko ya kwanza ya makundi na ng'ombe. Kwa maana maisha yao yatakuwa kama busitani iliyomwagiliwa, na hatatajisikia huzuni tena. 13Kisha wanawali watafurahia kwa kucheza, na vijana na wanaume wazee watakuwa pamaoja. Kwa maana nitayageuza maombolezo yao kuwa sherehe. Nitakuwa na huruma juu yao na kuwafanya kufurahi badala ya kuhuzunika.
Injili
43Wote walishangazwa na ukuu wa Mungu. Lakini walipokuwa wakistaajabu wote kwa mambo yote aliyo yaliyotedeka, akasema kwa wanafunzi wake, 44“Maneno yawakae masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu atatolewa mikononi mwa wanadamu.” 45Lakni hawakuelewa maana ya maneno hayo, na yalifichwa machoni pao, ili wasije wakalielewa. Waliogopa kumuuliza kuhusu neno hilo.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki