Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 23 Septemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 23 Septemba 2027

Alhamisi · Juma la 25 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 25 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Pio wa Pietrelcina (Padre Pio), padre · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Hag 1:1–8

1Katika mwaka wa pili wa mfalme Dario, katika mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana likaja kwa kwa mkono wa nabii Haghai kwenda kwa gavana wa Yuda, Zerubabeli mwana wa Sheatieli na kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki, kusema, 2“Bwana wa Majeshi asema: 'Hawa watu husema, “Si wakati wetu kuja au kujenga nyumba ya Jehova."”” 3Tena neno la Bwana lilikuja kwa mkono wa nabii Haghai kusema, 4“Je ni wakati kwenu wenyewe kuishi katika nyumba zilizokamilika, na wakati nyumba hii inaharibika? 5Kwa hiyo sasa Bwana wa Majeshi asema hivi: 'zitafakarini njia zenu! 6Mmepanda mbengu nyingi, lakini mkaleta mavuno kidogo; mnakula lakini hamshibi, mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji. Mnavaa nguo lakini hampati joto wenyewe, na mtu wa mshahara hupata pesa na kuweka kwenye mfuko wenye mashimo tu!' 7Bwana wa Majeshi asema haya: 8'Zitafakarini njia zetu! Pandeni milimani, mkalete mbao, na mjenge nyumba yangu; na pia nitakuwa radhi na nitatukuzwa!' Asema Bwana.

Wimbo wa katikati

Zab 149:1–6, 9

1Msifuni Yahwe. Mwimbieni Yahwe wimbo mpya; imbeni sifa zake katika kusanyiko la waaminifu. 2Israeli ishangilie katika yeye aliye iumba; watu wa Sayuni na washangilie katika mfalme wao. 3Nao walisifu jina lake kwa kucheza; na wamuimbie sifa yeye kwa ngoma na kinubi. 4Kwa kuwa Yahwe hupata furaha katika watu wake; huwapa utukufu wanyeyekevu kwa wokovu. 5Wacha Mungu wauchangilie ushindi; nao waimbe kwa furaha vitandani mwao. 6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na panga mbili zenye makali mkononi mwao 9Hii itakuwa ni heshima kwa ajili ya watakatifu wake wote. Msifuni Yahwe.

Injili

Lk 9:7–9

7Sasa Herode, mtawala, alisikia yote yaliyo kuwa yakitokea alitaabika sana, kwa sababuu ilisemekana na baadhi kwamba Yohana mbatizaji amefufuka kutoka wafu, 8na baathi kwamba Elia amekwisha tokea, na kwa wengine kwamba mmoja wa manabii wa zamani amefufuka katika wafu tena. 9Herode alisema, “nilimchinja Yohana, lakini huyu ni nani ninae sikia habari zake? Na Herode alitafuta njia ya kumwona Yesu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 23 Septemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki