Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 16 Septemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 16 Septemba 2027

Alhamisi · Juma la 24 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 24 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Watakatifu Kornelio, papa, na Sipriani, askofu, mashahidi · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

1 Tim 4:12–16

12Mtu yeyote asiudharau ujana wako. Badala yake, uwe mfano kwa wote waaminio, katika usemi, mwenendo, upendo, uaminifu, na usafi. 13Mpaka nitakapokuja, dumu katika kusoma, katika kuonya, na katika kufundisha. 14Usiipuuze karama iliyomo ndani yako, ambayo ulipewa kupitia unabii, kwa kuwekewa mikono na wazee. 15Uyajali mambo haya. Ishi katika hayo ili kukua kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. Zingatia sana mwenendo wako na mafundisho. 16Dumu katika mambo haya. Maana kwa kufanya hivyo utajiokoa mwenyewe na wale wanaokusikiliza.

Wimbo wa katikati

Zab 111:7–10

7Kazi za mikono yake ni za kuaminika na haki; maagizo yake yote ni ya kuaminika. 8Yamethibitika milele, yamefanywa katika uaminifu na vizuri. 9Aliwapa ushindi watu wake; aliliteuwa agano lake milele; jina lake ni takatifu na lakutisha. 10Kumcha Yahwe ni mwanzo wa hekima; wale washikao maagizo yake wana uelewa mzuri. Sifa yake yadumu milele.

Injili

Lk 7:36–50

36Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale. 37Tazama kulikuwa na mwanamke mmoja katika jiji hilo aliyekuwa na dhambi. Akagundua kuwa alikuwa amekaa kwa Farisayo, akaleta chupa ya manukato. 38Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato. 39Na yule farisayo aliyekuwa amemwalika Yesu alipoona hivyo, akawaza mwenyewe akisema, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua huyu ni nani na ni aina gani ya mwanamke anayemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi. 40Yesu akajibu na kumwambia, “Simoni nina kitu cha kukuambia. “Akasema” “Kiseme tu mwalimu!” 41Yesu akasema “Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini. 42Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi? 43Simoni akamjibu na kusema, “Nadhani aliyesamehewa zaidi.”Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.” 44Yesu akamgeukia mwanamke na kusema kwa Simoni, “Unamwona huyu mwanamke. Nimeingia kwenye Nyumba yako. Hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu, lakini huyu, kwa machozi yake, alilowanisha miguu yangu na kuifuta kwa nywele zake. 45Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu. 46Hukuipaka miguu yangu kwa mafuta, lakini ameipaka miguu yangu kwa manukato. 47Kwa jambo hili, nakwambia kwamba alikuwa na dhambi nyingi na amesamehewa zaidi, na pia alipenda zaidi. Lakini aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo tu.” 48Baadaye akamwambia mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa” 49Wale waliokaa mezani pamoja naye wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani mpaka anasamehe dhambi?” 50Na Yesu akamwambia mwanamke, “Imani yako imekuokoa. Enenda kwa amani”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 16 Septemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki