Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 15 Septemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 15 Septemba 2027

Jumatano · Juma la 24 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 24 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Bikira Maria wa Mateso · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

1 Tim 3:14–16

14Ninaandika mambo haya kwako, na ninatumaini kuja kwako hivi karibuni. 15Lakini ikiwa nitachelewa, ninaandika ili upate kujua namna ya kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambalo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msaada wa kweli. 16Na haipingiki kwamba kweli ya Uungu uliyofunuliwa ni mkuu: “Alionekana katika mwili, akathibitishwa na Roho, akaonekana na malaika, akatangazwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa na ulimwengu, na akachukuliwa juu katika utukufu.”

Wimbo wa katikati

Zab 111:1–6

1Msifuni Yahwe. Nitamshukuru Yahwe kwa moyo wangu wote katikati ya kusanyiko la wanye haki, na katika mkutano. 2Kazi za Yahwe ni kuu, zikisubiriwa na wale wazitamanio. 3Kazi yake ni adhama na utukufu, na haki yake yadumu milele. 4Hufanya mambo makuu ambayo yatakumbukwa; Yahwe ni mwenye huruma na neema. 5Huwapa chakula wafuasi wake waaminifu. Siku zote atalikumbuka agano lake. 6Alionesha uweza wa kazi zake kwa watu wake kwa kuwapa urithi wa mataifa.

Injili

Yn 19:25–27

au: Lk 2:33–35

25Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu. 26Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!” 27Kisha akamwambia yule mwanfunzi, “Tazama, huyu hapa mama yako. “Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.

Watakatifu wa 15 Septemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki