Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 16 Septemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 3 Septemba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 16 Septemba 2027

Alhamisi · Wiki ya 13 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3

Sikukuu na watakatifu

Mfiadini wa Kikasisi Anthimo, Askofu wa Nikomedia, na pamoja naye Wafiadini Theofilo, shemasi, Dorotheo, Mardonio, Migdonio, Petro, Indi, Gorgonio, Zenoni, Domna bikira na Euthimio (302)

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

2 Kor 10:7–18

7Tazama kile kilichowazi mbele yenu. Kama yeyote anashawishika kwamba yeye ni wa Kristo, na hebu ajikumbushe yeye mwenyewe kwamba kama tu alivyo ni wa Kristo, hivyo ndiyo na sisi pia tuko hivyo. 8Kwa kuwa hata nikijivuna kidogo zaidi kuhusu mamlaka yetu, ambayo Bwana aliyatoa kwa ajili yetu kuwajenga ninyi na siyo kuwaharibu, sitaona haya. 9Sihitaji hili lionekane kwamba nawatisha ninyi kwa nyaraka zangu. 10Kwa vile baadhi ya watu husema, “ Nyaraka zake ni kali na zina nguvu, lakini kimwili yeye ni dhaifu. Maneno yake hayastahili kusikilizwa.” 11Hebu watu wa jinsi hiyo waelewe kwamba kile tusemacho kwa waraka wakati tukiwa mbali, ni sawasawa na vile tutakavyotenda wakati tukiwa pale. 12Hatuendi mbali mno kama kujikusanya wenyewe au kujilinganisha wenyewe na wale ambao hujisifia wenyewe. Lakini wanapojipima wenyewe na kila mmoja wao, hawana akili. 13Sisi, hata hivyo, hatutajivuna kupita mipaka. Badala yake, tutafanya hivyo tu ndani ya mipaka ambayo Mungu ametupimia sisi, mipaka inayofika umbali kama wenu ulivyo. 14Kwa kuwa hatukujizidishia wenyewe tulipowafikia ninyi. Tulikuwa wa kwanza kufika kwa umbali kama wenu kwa injili ya Kristo. 15Hatujajivuna kupita mipaka kuhusu kazi za wengine. Badala yake, tunatumaini kama imani yenu ikuwavyo kwamba eneo letu la kazi litapanuliwa sana, na bado ni ndani ya mipaka sahihi. 16Tunatumaini kwa hili, ili kwamba tuweze kuhubiri injili hata kwenye mikoa zaidi yenu. Hatutajivuna kuhusu kazi inayofanywa katika maeneo mengine. 17“Lakini yeyote ajivunaye, ajivune katika Bwana.” 18Kwa maana siyo yule ajithibitishaye mwenyewe anathibitishwa. Isipokuwa, ni yule ambaye Bwana humthibitisha.

Injili

Mk 3:28–35

28Kweli nawambieni, dhambi zote za wana wa watu zitasamehewa, pamoja na kufuru ambazo wanatamka, 29lakini yeyote atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, bali ana hatia ya dhambi ya milele”. 30Yesu alilisema hili kwa sababu walikuwa wakisema, “Ana roho chafu”. 31Kisha mama yake na ndugu zake walikuja na kusimama nje. Wakamtuma mtu, kumwita. 32Na umati wa watu uliokuwa umekaa karibu naye wakamwambia, “mama yako na ndugu zako wako nje, na wanakutafuta wewe”. 33Aliwajibu, “Ni nani mama yangu na ndugu zangu?” 34Aliwaangalia waliokuwa wamekaa wamemzunguka, na akasema, “Tazama, hawa ni mama zangu na ndugu zangu! 35Yeyote afanyaye mapenzi ya Mungu, mtu huyo ni ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu”.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 16 Septemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 3 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 16 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki