Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 9 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 27 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 9 Septemba 2027
Alhamisi · Wiki ya 12 baada ya Pentekoste · Sauti ya 2
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Pimeni Mkuu (karibu 450)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Wapendwa wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizi, na tujitakase wenyewe kwa kila jambo ambalo linatufanya kuwa wachafu katika miili yetu na katika roho. Na tuutafute utakatifu katika hofu ya Mungu. 2Fanyeni nafasi kwa ajili yetu! Hatujamkosea mtu yeyote. Hatukumdhuru mtu yeyote. Hatujajinufaisha kwa faida ya mtu yeyote. 3Nasema hili siyo kwa kuwalaumu. Kwa kuwa nimeshasema kwamba mmo mioyoni mwetu, kwetu sisi kufa pamoja na kuishi pamoja. 4Nina ujasiri mwingi ndani yenu, na ninajivuna kwa ajili yenu. Nimejawa na faraja. Ninajawa na furaha hata katikati ya mateso yetu yote. 5Tulikuja Makedonia, miili yetu haikuwa na pumziko. Badala yake, tulipata taabu kwa namna zote kwa kupigwa vita upande wa nje na hofu upande wa ndani. 6Lakini Mungu, anayefariji waliokata tamaa, alitufariji kwa ujio wa Tito. 7Haikuwa kwa ujio wake tu kwamba Mungu alitufariji. ilikuwa pia faraja zile Tito alizopokea kutoka kwenu. Yeye alituambia upendo mkuu mlionao, huzuni yenu, na mlivyokuwa na wasiwasi kwa ajili yangu. Hivyo nimezidi kuwa na furaha zaidi. 8Hata ingawa waraka wangu uliwafanya kusikitika, mimi siujutii. lakini ninaujutia wakati nilipoona waraka huo uliwafanya ninyi kuwa na huzuni. lakini mlikuwa na huzuni kwa muda mfupi. 9Sasa nina furaha, si kwa sababu mlikuwa na shida, lakini kwa sababu huzuni zenu iliwaleta kwenye toba. Mlipatwa na huzuni ya kiungu, hivyo mliteswa si kwa hasara kwa sababu yetu. 10Kwa kuwa huzuni ya kiungu huleta toba ambayo hukamilisha wokovu bila ya kuwa na majuto. Huzuni ya kidunia, hata hivyo, huleta mauti.
Injili
29Na mara moja baada ya kutoka nje ya sinagogi, waliingia nyumbani mwa Simoni na Andrea wakiwa na Yakobo na Yohana. 30Sasa mama mkwe wa Simoni alikuwa amelala mgonjwa wa homa, na mara moja walimwambia Yesu habari zake. 31Hivyo alikuja, alimshika kwa mkono, na kumwinua juu; homa ikaondoka kwake, na akaanza kuwahudumia. 32Jioni hiyo wakati jua limekwisha zama, walimletea kwake wote waliokuwa wagonjwa, au waliopagawa na pepo. 33Mji wote walikusanyika pamoja katika mlango. 34Aliwaponya wengi waliokuwa wagonjwa wa magonjwa mbalimbali na kutoa pepo wengi, bali hakuruhusu pepo kuongea kwa sababu walimjua. 35Aliamka asubuhi na mapema, wakati ilikuwa bado giza; aliondoka na kwenda mahali pa faragha na aliomba huko.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Mikaeli, padri, na pamoja naye wafiadini 28 (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Stefano, padri, na pamoja naye wafiadini 18 (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Yohana na Yohana, mapadri, na Mtawa Mfiadini Methodio (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, padri (1939)
- Mfiadini wa Kikasisi Vladimir, padri (1940)
- Mtakatifu Demetrio Mwungamaji, padri (1952)
- Askofu Mtakatifu Hosio Mwungamaji, Askofu wa Kordoba (359)
- Askofu Mtakatifu Liberio Mwungamaji, Papa wa Roma (366)
- Mtakatifu Mtawa Pimeni wa Palestina (karibu 602)
- Watakatifu Watawa wa Mapango ya Kyiv: Mfiadini wa Kikasisi Kuksha na mwanafunzi wake Mfiadini Nikoni, na Mtakatifu Mtawa Pimeni, mfungaji (baada ya 1114)
- Mtakatifu Mtawa Sava
- Mfiadini Anthusa Mpya
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 27 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 9 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki