Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 3 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 21 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 3 Septemba 2027
Ijumaa · Wiki ya 11 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kulala kwa Mama Mtakatifu Sana wa Mungu
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
13Lakini tuna roho ileile ya imani kulingana na kile kilicho andikwa: “Niliamini, na hivyo nilinena.” Sisi pia tunaamini, na hivyo pia tunanena. 14Tunajua kuwa yule aliye mfufua Bwana Yesu pia atatufufua sisi pamoja naye. Tunajua kuwa atatuleta sisi pamoja nanyi katika uwepo wake. 15Kila kitu ni kwa ajili yenu ili kwamba, kwa kadri neema inavyo enea kwa watu wengi, shukurani zizidi kuongezeka kwa utukufu wa Mungu. 16Hivyo hatukati tamaa. Japokuwa kwa nje tunachakaa, kwa ndani tunafanywa upya siku hadi siku. 17Kwa kipindi hiki kifupi, mateso haya mepesi yanatuandaa sisi kwa ajili ya umilele mzito wa utukufu uzidio vipimo vyote. 18Kwa kuwa hatutazami kwa ajili ya vitu ambavyo vinaonekana, bali kwa ajili ya vitu visivyoonekana. Vitu tunavyoweza kuviona ni vya muda tu, bali vitu ambayo havionekani ni vya milele.
Injili
27Kama vile radi inavyomulika kutokea mashariki na kuangaza hadi magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu. 28Popote ulipo mzoga, huko ndiko tai wakusanyikapo. 29Lakini mara baada ya dhiki kuu ya siku zile, Jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbinguni zitatikisika. 30Ndipo ishara ya Mwana wa Adamu itaonekana angani, na makabila yote ya dunia wataomboleza. Watamwona Mwana wa Adamu akija katika mawingu ya angani kwa nguvu na utukufu mkuu. 31Atawatuma malaika wake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwingine. 32Jifunzeni somo kutokana na mti mtini. Mara tu tawi linapochipuka na kutoa majani, mnajua kwamba kiangazi kinakaribia. 33Hivyo pia, mtakapoona mambo haya yote, mnapaswa kujua kwamba amekaribia, karibu na malango. 42Kwa hiyo, kuweni macho kwa sababu hamjui ni siku gani ambayo atakuja Bwana wenu. 43Lakini mjue kwamba, ikiwa bwana mwenye nyumba angejua ni saa ipi ambayo mwizi angekuja, angekesha na asingeruhusu nyumba yake kuvamiwa. 44Kwa hiyo, pia mnapaswa kuwa tayari, kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika saa msiyoitarajia. 45Hivyo ni nani aliye mwaminifu, mtumwa mwenye akili, ambaye bwana wake amempa madaraka juu ya walio katika nyumba yake, ili awape chakula kwa wakati unaofaa? 46Amebarikiwa mtumishi huyo, ambaye bwana wake atamkuta akifanya hivyo wakati ajapo. 47Kweli nawaambia kwamba bwana atamweka juu ya kila kitu kilicho chake. 48Lakini kama mtumwa mwovu akisema moyoni mwake, 'Bwana wangu amekawia,' 49na akaanza kuwapiga watumishi wake, na akala na kulewa vileo, 50Bwana wa mtumwa huyo atakuja katika siku ambayo haitarajii, na katika saa ambayo haijui. 51Bwana wake atamkata vipande viwili na kumweka katika nafasi moja sawa na wanafiki, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
Watakatifu wa siku
- Mtume Thadayo, wa Mitume 70 (karibu 44)
- Mfiadini Basa na watoto wake, Wafiadini Theognio, Agapio na Pisto (305-311)
- Mtakatifu Mtawa Ibrahimu wa Smolensk (kabla ya 1224)
- Mtakatifu Mtawa Martha wa Diveyevo (1829)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, padri (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Paulo, padri (1937)
- Mtawa Mfiadini Ignatio (1942)
- Mtakatifu Mtawa Ibrahimu, mwenye bidii ya kazi, wa Mapango ya Kyiv (karne ya 12-13)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 21 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 3 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki