Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 4 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 22 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 4 Septemba 2027
Jumamosi · Wiki ya 11 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kulala kwa Mama Mtakatifu Sana wa Mungu
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
3Neema na amani iwe kwenu kutoka kwa Mungu baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo. 4Siku zote namshukru Mungu wangu kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu ambayo Kristo Yesu aliwapa. 5Amewafanya kuwa matajiri katika kila njia, katika usemi na pamoja maarifa yote. 6Amewafanya matajiri, kama ushuhuda kuhusu Kristo ya kwamba amethibitishwa kuwa kweli miongoni mwenu. 7Kwa hiyo hampungukiwi karama za kiroho, kama mlivyo na hamu ya kusubiri ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo. 8Atawaimarisha ninyi pia hadi mwisho, ili msilaumiwe siku ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita ninyi katika ushirika wa mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.
Injili
3Mafarisayo wakamjia, wakamjaribu, wakamwambia, “Je ni halali kwa mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?” 4Yesu akajibu na kusema, “Hamkusoma, kwamba yeye aliyewaumba mwanzo aliwaumba mume na mke? 5Na tena akasema, 'Kwa sababu hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?' 6Hivyo siyo wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, kile alichokiunganisha Mungu, mtu yeyote asikitenganishe.” 7Wakamwambia, “Sasa kwa nini Musa alituamuru kutoa hati ya talaka na kumwacha?” 8Akawaambia, “Kwa ugumu wenu wa mioyo Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu, lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo. 9Nawaambieni, kwamba yeyote atayemwacha mke wake, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, na akamwoa mwingine, amezini. Na mwanaume atakayemwoa mke aliyeachwa amezini.” 10Wanafunzi wakamwambia Yesu, “Kama ndivyo ilivyo kwa mume na mkewe, siyo vizuri kuoa.” 11Lakini Yesu akawaambia, “Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya, bali ni kwa wale tu walioruhusiwa kupokea. 12Kwa vile wapo matowashi waliozaliwa tokea tumboni mwa mama zao. Na vilevile kuna matowashi waliofanywa na watu. Na kuna matowashi waliojifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kupokea mafundisho haya na ayapokee.”
Watakatifu wa siku
- Wafiadini Agathoniko, Zotiko, Theoprepio, Akindino, Severiani na wengine (305-311)
- Mtakatifu Mtawa Isaka I wa Optina (1894)
- Mfiadini wa Kikasisi Gorazd, Askofu wa Bohemia na Moravia-Silesia (1942)
- Wafiadini wa Kikasisi Makario, Askofu wa Oryol, Yohana na Aleksi, mapadri (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Theodoro, Askofu wa Penza, na pamoja naye Basili na Gabrieli, mapadri (1937)
- Wafiadini wa Kikasisi Yohana, Askofu wa Velikiye Luki, Aleksi, Askofu Mkuu wa Omsk, Aleksanda, Mikaeli na Theodoro, mapadri, Watawa Wafiadini Hilarioni, Yohana na Hierotheo (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Athanasio, Askofu wa Tarso ya Kilikia (270-275), Mtakatifu Mtawa Anthusa (karibu 298) na watumishi wake, Wafiadini Kharisimo na Neofito (270-275)
- Mfiadini Eulalia, bikira (karibu 303)
- Ikoni ya Mama wa Mungu ya Georgia (1650)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 22 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 4 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki