Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 2 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 20 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 2 Septemba 2027
Alhamisi · Wiki ya 11 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kulala kwa Mama Mtakatifu Sana wa Mungu
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Kwa hiyo, kwa sababu tuna huduma hii, na kama ambavyo tumeipokea rehema, hatukati tamaa. 2Badala yake, tumekataa njia zote za aibu na zilizofichika. Hatuishi kwa hila, na hatulitumii vibaya neno la Mungu. Kwa kuwasilisha iliyo kweli, tunajionyesha wenyewe kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu. 3Lakini kama injili yetu imefichika, imefichika kwa wale tu wanaoangamia. 4Katika uchaguzi wao, mungu wa ulimwengu huu amewapofusha fahamu zao zisizoamini. Matokeo yake, hawawezi kuona nuru ya injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano wa Mungu. 5Kwa kuwa hatujitangazi wenyewe, bali Kristo Yesu kama Bwana, na sisi wenyewe kama watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6Kwa kuwa Mungu ndiye ambaye aliyesema, “Mwanga utaangaza toka gizani.” Ameangaza katika mioyo yetu, kutoa mwanga wa maarifa ya utukufu wa Mungu katika uwepo wa Yesu Kristo.
Injili
13Lakini atakaye vumilia mpaka mwisho, ataokolewa. 14Hii Injili ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu mzima kama ushuhuda kwa mataifa yote. Na ndipo ule mwisho utafika. 15Kwa hiyo, mtakapoona chukizo la uharibifu, lililosemwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu [asomaye na afahamu], 16ndipo walioko Yuda wakimbilie milimani. 17Na yule aliyeko juu ya paa la nyumba asiweze kuteremka chini kuchukua kitu chochote kutoka ndani ya nyumba yake, 18naye aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake. 19Lakini ole wao ambao wana mtoto na wale ambao wananyonyesha katika siku hizo! 20Ombeni kwamba kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. 21Kwa kuwa kutakuwa na dhiki kuu, ambayo haijawahi kuwapo tangu kuumbwa kwa ulimwengu hadi sasa, na wala haitakuwapo tena. 22Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna ambaye angeokoka. Lakini kwa sababu ya wateule, siku hizo zitafupishwa. 23Kisha ikiwa mtu yeyote atawaambia 'Tazama, Kristo yuko hapa! au, 'Kristo yuko kule' msiamini maneno hayo. 24Kwa kuwa Makristo wa uongo na manabii wa uongo watakuja na kuonesha ishara kubwa na maajabu, kwa kusudi la kupotosha, kama ingewezekana hata na wateule. 25Tazameni, nimewatahadharisha kabla ya mambo hayo kutokea. 26Kwa hiyo, ikiwa watawaambia, ''Kristo yuko jangwani,' msiende huko jangwani. Au, 'Tazameni, yuko ndani ya nyumba,' msiamini maneno hayo. 27Kama vile radi inavyomulika kutokea mashariki na kuangaza hadi magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu. 28Popote ulipo mzoga, huko ndiko tai wakusanyikapo.
Watakatifu wa siku
- Nabii Samweli (karne ya 11 K.K.)
- Mfiadini wa Kikasisi Vladimir, padri (1917)
- Wafiadini Severo na Memnoni na pamoja nao wafiadini 37 (304)
- Askofu Mtakatifu Hierotheo wa Hungaria (karne ya 10) na Mtakatifu Stefano I, mfalme wa Hungaria (1038)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 20 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 2 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki