Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 17 Agosti

Kalenda ya Kiorthodoksi · 4 Agosti (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 17 Agosti 2027

Jumanne · Wiki ya 9 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7

Sikukuu na watakatifu

Vijana saba wa Efeso: Maksimiliani, Iamblika, Martiniani, Yohana, Dionisio, Eksakustodiani (Konstantino) na Antonino (karibu 250, 408-450)

Mfungo wa Kulala kwa Mama wa Mungu

Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

1 Kor 12:12–26

12Kwa maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote ni vya mwili ule ule, vivyo hivyo na Kristo. 13Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi au Wayunani, kwamba tu watumwa au huru, na wote tulinyweshwa Roho mmoja. 14Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. 15Ikiwa mguu utasema, “kwa kuwa mimi si mkono, mimi si sehemu ya mwili,” hiyo haiufanyi kutokuwa sehemu ya mwili. 16Na ikiwa sikio litasema, “kwa kuwa mimi si jicho, mimi si sehemu ya mwili,” hiyo hailifanyi kutokuwa sehemu ya mwili. 17Kama mwili wote utakuwa jicho, kungekuwa wapi kusikia? Kama mwili wote ukiwa sikio, kungekuwa wapi kunusa? 18Lakini Mungu aliweka kila kiungo cha mwili mahali pake kama alivyopanga mwenyewe. 19Na kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? 20Hivyo sasa viungo ni vingi, lakini mwili ni mmoja. 21Jicho haliwezi kuuambia mkono, “sina haja na wewe.” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja na ninyi.” 22Lakini viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa na heshima kidogo vyahitajika zaidi. 23Na viungo vya mwili tunavyodhani vina heshima kidogo, twavipa heshima zaidi, na viungo vyetu visivyo na mvuto vina uzuri zaidi. 24Na sasa viungo vyetu vilivyo na mvuto havina haja ya kupewa heshima, kwa kuwa tayari vina heshima. Lakini Mungu ameviunganisha viungo vyote pamoja, na amevipa heshima zaidi vile visivyo heshimiwa. 25Alifanya hivyo ili pasiwepo mgawanyiko katika mwili, bali viungo vyote vitunzane kwa upendo wa mmoja. 26Na wakati kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote vyaumia kwa pamoja. Au wakati kiungo kimoja kikiheshimiwa, viungo vyote vifurahi kwa pamoja.

Injili

Mt 18:18–22; 19:1–2, 13–15

18Kweli nawaambieni, chochote kile mtakachokifunga duniani na mbinguni kitafungwa. na chochote mtakachokifungua duniani na mbinguni kitafunguliwa. 19Tena nawaambieni kwamba kama watu wawili kati yenu wakikubaliana juu ya jambo lolote duniani waliombalo, hilo Baba yangu wa mbinguni atalifanya. 20Kwa kuwa wawili au watatu wakikusanyika pamoja kwa jina langu, Mimi niko katikati yao. 21Tena Petro akaja na kumwambia Yesu, “Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu akinikosea nami nimsamehe? Hata mara saba?” 22Yesu akamwambia, “Sikuambii mara saba, lakini hata sabini mara saba. 19:1Ilitokea wakati Yesu alipomaliza maneno hayo, akaondoka Galilaya, na akaenda mpakani mwa Yudea mbele ya mto Jordani. 2Umati mkubwa ukamfuata, na akawaponya huko. 13Kisha akaletewa baadhi ya watoto wadogo ili awawekee mikono juu yao na kuomba, lakini wanafunzi wake wakawakemea. 14Bali Yesu akasema, “Waruhusuni watoto wadogo, wala msiwakataze kuja kwangu, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa watu kama wao. 15Naye akaweka mikono yake juu yao, na kisha akaondoka pale.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 17 Agosti

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 4 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 17 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki