Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 13 Agosti

Kalenda ya Kiorthodoksi · 31 Julai (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 13 Agosti 2027

Ijumaa · Wiki ya 8 baada ya Pentekoste · Sauti ya 6

Sikukuu na watakatifu

Kabla ya Sikukuu ya Kutolewa kwa miti yenye thamani ya Msalaba Utoao Uzima wa Bwana

Siku ya mfungo

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

1 Kor 11:8–22

8Maana mwanamume hakutokana na mwanamke. Bali mwanamke alitokana na mwanamume. 9Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke. Bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume. 10Hii ndio sababu mwanamke anapaswa kuwa na ishara ya mamlaka juu ya kichwa chake, kwa sababu ya malaika. 11Hata hivyo, katika Bwana, mwanamke hayupo peke yake pasipo mwanamume, au mwanamume pasipo mwanamke. 12Maana kama vile mwanamke alitoka kwa mwanamume, vile vile mwanamume alitoka kwa mwanamke. Na vitu vyote hutoka kwa Mungu. 13Hukumuni wenyewe: Je! ni sahihi mwanamke amuombe Mungu hali kichwa chake kikiwa wazi? 14Je hata asili peke yake haiwafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake? 15Je asili haiwafundishi ya kwamba mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake? Maana amepewa zile nywele ndefu kama vazi lake. 16Lakini ikiwa mtu yeyote anataka kubishana juu ya hili, sisi hatuna namna nyingine, wala makanisa ya Mungu. 17Katika maagizo yafuatayo, mimi siwasifu. Maana mnapokusanyika, sio kwa faida bali kwa hasara. 18Maana kwanza, nasikia ya kuwa mkutanikapo kanisani, kuna migawanyiko kati yenu, na kwa sehemu ninaamini. 19Kwa maana ni lazima iwepo misuguano kati yenu, ili kwamba wale waliokubaliwa wajulikane kwenu. 20Kwa maana mkutanikapo, mnachokula sio chakula cha Bwana. 21Mnapokula, kila mmoja hula chakula chake mwenyewe kabla wengine hawajala. hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. 22Je hamna nyumba za kulia na kunywea? Je mnalidharau kanisa la Mungu na kuwafedhehesha wasio na Kitu? Niseme nini kwenu? Niwasifu? Sitawasifu katika hili!

Waraka (ya Jumamosi)

Rum 13:1–10

1Kila nafsi na iwe na utii kwa mamlaka ya juu, kwa kuwa hakuna mamlaka isipokuwa imetoka kwa Mungu. Na mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu. 2Kwa hiyo ambaye anapinga mamlaka hiyo hupinga amri ya Mungu; na wale waipingao watapokea hukumu juu yao wenyewe. 3Kwa kuwa watawala si tishio kwa watendao mema, bali kwa watendao maovu. Je unatamani kutoogopa mamlaka? Fanya yaliyo mema, na utasifiwa nayo. 4Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Bali kama utatenda yaliyo maovu, ogopa; kwa kuwa habebi upanga bila sababu. Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, mlipa kisasi kwa ghadhabu juu ya yule afanyaye uovu. 5Kwa hiyo inakupasa utii, si tu kwa sababu ya gadhabu, bali pia kwa sababu ya dhamiri. 6Kwa ajili hii pia unalipa kodi. Kwa kuwa wenye mamlaka ni watumishi wa Mungu, ambao wanaendelea kufanya jambo hili. 7Mlipeni kila mmoja ambacho wanawadai: kodi kwa astahiliye kodi; ushuru kwa astahiliye ushuru; hofu kwa astahiliye hofu; heshima kwa astahiliye heshima. 8Msidaiwe na mtu kitu chochote, isipokuwa kupendana ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa yeye ampendaye jirani yake ametimiliza sheria. 9Kwa kuwa, “Hautazini, hautaua, hautaiba, hautatamani,” na kama kuna amri nyingine pia, imejumlishwa katika sentensi hii: “Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe.” 10Upendo hamdhuru jirani wa mtu. Kwa hiyo, upendo ni ukamilifu wa sheria.

Injili

Mt 17:10–18

10Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, “ Ni kwanini waandishi wanasema kuwa Eliya atakuja kwanza? 11Yesu akawajibu na kusema, “Eliya atakuja kweli na atarudisha mambo yote. 12Lakini naawaambieni ninyi, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua. Badala yake, walimfanyia mambo watakayo wao. Na hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyoteswa katika mikono yao.” 13Ndipo wanafunzi wakatambua kuwa alikuwa akiongea habari za Yohana Mbatizaji. 14Walipofika katika umati wa watu, mtu mmoja alimwendea, akapiga magoti mbele zake, na kumwambia, 15“Bwana, umhurumie mwanangu, maana amekuwa na kifafa na kuteseka sana. Kwa kuwa mara nyingi huanguka motoni au kwenye maji. 16Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya. 17Yesu akajibu akisema, “Enyi Kizazi kisichoamini na kilichoharibika, nitakaa pamoja nanyi mpaka lini? Nitavumiliana nanyi hata lini? Mlete hapa kwangu.” 18Yesu alimkemea, na pepo akamtoka. Kijana aliponywa tangu saa ile.

Injili (ya Jumamosi)

Mt 12:30–37

30Yeyote asiye kuwa pamoja nami yuko kinyume changu, naye asiye kusanya pamoja nami huyo hutawanya. 31Kwa hiyo nasema kwenu, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, ila kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa. 32Na yeyote asemaye neno kinyume cha Mwana wa Adamu, hilo atasamehewa. Lakini yeyote asemaye kinyume na Roho Mtakatifu, huyo hatasamehewa, katika ulimwengu huu, na wala ule ujao 33Ama ufanye mti kuwa mzuri na tunda lake zuri, au uuharibu mti na tunda lake, kwa kuwa mti hutambulika kwa tunda lake. 34Nyinyi kizazi cha nyoka, nyie ni waovu, mnawezaje kusema mambo mazuri? Kwa kuwa kinywa hunena kutoka katika akiba ya yaliyomo moyoni. 35Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoka mema, na mtu mwovu katika akiba ovu ya moyo wake, hutoa kilicho kiovu. 36Nawaambia kuwa katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu ya kila neno lisilo na maana walilosema. 37Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 13 Agosti

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 31 Julai katika kalenda ya kanisa ni 13 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki