Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 11 Agosti
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 11 Agosti 2027
Jumatano · Juma la 19 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatano ya Juma la 19 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Klara, bikira · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Musa aliondoka kutoka nyanda za Moabu mpaka mlima wa Nebo, hadi kilele cha Pisga, kilicho mkabala na Yericho. Huko Yahwe alimwonyesha nchi yote ya Gileadi kutoka umbali wa Dani, 2na Naftali yote, na nchi ya Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda, mpaka bahari ya magharibi, 3na Negevi, na uwanda wa bonde la Yericho, mji wa mitende, mpaka umbali wa Soari. 4Yahwe alimwambia, “Hii ni nchi niliyoapa kwa Abrahamu, kwa Isaka, na kwa Yakobo, na kusema, “Nitawapatia uzao wako. ” Nimekuruhusu uitazame kwa macho yako, lakini hautakwenda kule. ” 5Basi Musa mtumishi wa Yahwe, alikufa pale katika nchi ya Moabu, kama neno la Yahwe lilivyoahidi. 6Yahwe alimzika katika bonde katika nchi ya Moabu mkabala na Beth-peori, lakini hakuna ajuaye kaburi lake lilipo hadi leo hii. 7Musa alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipokufa; macho yake hayakufifia, wala nguvu asili zake hazikupungua. 8Watu wa Israeli walimuomboleza Musa katika nyanda za Moabu kwa siku thelathini, hapo ndipo siku za maombolezo ya Musa zilipotimia. 9Yoshua mwana wa Nuni alikuwa amejawa na roho ya hekima, kwa maana Musa alimwekea mkono juu yake. Watu wa Israeli walimsikiliza na kufanya yale ambayo Yahwe alimuamuru Musa. 10Tangu hapo hakujatokea nabii katika Israeli kama Musa, ambaye Yahwe alimjua uso kwa uso. 11Hakujawahi kuwa na nabii yeyote kama yeye kwa ishara na miujiza ambayo Yahwe alimtuma kufanya katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake, na kwa nchi yake yote. 12Hakujawahi kuwa na nabii yeyote kama yeye kwa mambo yote makubwa, ya kutisha ambayo Musa aliyafanya machoni pa Israeli yote.
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki. Wimbo, Zaburi. Mpigieni Mungu kelele za shangwe, nchi yote; 2Imbeni utukufu wa jina lake; mzitukuze sifa zake. 3Mwambieni Mugu, “Matendo yako yanatisha kama nini! Kwa ukuu wa nguvu zako maadui zako watajisalimisha kwako. 5Njoni na mtazame kazi za Mungu; yeye anatisha katika matendo yake awatendeayo wanadamu. 8Mtukuzeni Mungu, enyi watu wa mataifa yote, sauti ya sifa zake isikike. 16Njoni, msikie, ninyi nyote mnao mwabudu Mungu, nami nitatangaza yale yeye aliyoitendea roho yangu. 17Nilimlilia kwa kinywa changu, naye alipendezwa na ulimi wangu.
Injili
15Kama ndugu yako akikukosea, nenda, kamwonyeshe dosari iliyopo kati yako na yeye akiwa pekee yake. Kama akikusikiliza, utakuwa umemrejesha ndugu yako. 16Lakini kama hatakusikiliza, mchukue ndugu mmoja au wawili zaidi pamoja nawe, kwa kuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno linaweza kuthibitishwa. 17Na kama akipuuza kuwasikiliza, liambie kanisa jambo hilo, kama akipuuza vilevile kulisikiliza kanisa, basi na awe kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. 18Kweli nawaambieni, chochote kile mtakachokifunga duniani na mbinguni kitafungwa. na chochote mtakachokifungua duniani na mbinguni kitafunguliwa. 19Tena nawaambieni kwamba kama watu wawili kati yenu wakikubaliana juu ya jambo lolote duniani waliombalo, hilo Baba yangu wa mbinguni atalifanya. 20Kwa kuwa wawili au watatu wakikusanyika pamoja kwa jina langu, Mimi niko katikati yao.
Watakatifu wa siku
- Mt. Klara, bikira
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki