Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 10 Agosti
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 10 Agosti 2027
Jumanne · Juma la 19 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Mt. Laurenti, shemasi na shahidi
Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyekundu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
6Wazo ni hili: mtu apandaye haba pia atavuna haba, na yeyote apandaye kwa lengo la baraka pia atavuna baraka. 7Basi na kila mmoja atoe kama alivyopanga moyoni mwake. Basi naye asitoe kwa huzuni au kwa kulazimishwa. Kwa kuwa Mungu humpenda yule atoaye kwa furaha. 8Na Mungu anaweza kuizidishia kila baraka kwa ajili yenu, ili kwamba, kila wakati, katika mambo yote, muweze kupata yote mnayohitaji. Hii itakuwa ili kwamba mueze kuzidisha kila tendo jema. 9Ni kama ilivyoandikwa: “Ametapanya utajiri wake na kuutoa kwa maskini. Haki yake yadumu milele.” 10Naye atoaye mbegu kwa mpanzi na mkate kwa ajili ya chakula, pia atatoa na kuzidisha mbegu yenu kwa ajili ya kupanda. Yeye ataongeza mavuno ya haki yenu.
Wimbo wa katikati
1Msifuni Yahwe. Amebarikiwa mtu yule anaye mtii Yahwe, apendezwaye sana na amri zake. 2Kizazi chake kitakuwa ni chenye nguvu duniani; kizazi cha mcha Mungu kitabarikiwa. 5Heri atendaye fadhili na kukopesha, afanyaye mambo yake kwa uaminifu. 6Kwa maana hataondoshwa kamwe; mwenye haki atakumbukwa milele. 7Haogopi habari mbaya; ni jasiri, akimtumainia Yahwe. 8Moyo wake ni mtulivu, hana woga, mpaka aonapo ushindi dhidi ya watesi wake. 9Huwapa masikini kwa ukarimu; haki yake yadumu milele; atainuliwa kwa heshima.
Injili
24Amini, amini, nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka katika nchi ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, itazaa matunda mengi. 25Yeye apendaye uhai wake ataupoteza; bali yeye auchukiaye uhai wake katika ulimemngu huu atausalimisha hata uzima wa milele. 26Mtu yeyote akinitumikia mimi, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Mtu yeyote akinitumikia, Baba atamheshimu.
Watakatifu wa siku
- Mt. Laurenti, shemasi na shahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki