Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 10 Agosti

Kalenda ya Kiorthodoksi · 28 Julai (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 10 Agosti 2027

Jumanne · Wiki ya 8 baada ya Pentekoste · Sauti ya 6

Sikukuu na watakatifu

Mitume Prokoro, Nikanori, Timoni na Parmena, mashemasi, wa Mitume 70 (karne ya 1)

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

1 Kor 10:5–12

5Lakini Mungu hakupendezwa sana na wengi wao, na maiti zao zilisambazwa jangwani. 6Basi mambo haya yote yalikuwa mifano kwetu, ili sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya kama na wao walivyofanya. 7Msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa. Hii ni kama ilivyoandikwa, “Watu walikaa chini wakila na kunywa, na waliinuka kucheza kwa tamaa za mapenzi.” 8Tusifanye uasherati kama wengi wao walivyofanya. Wakafa siku moja watu ishirini na tatu elfu kwa sababu hiyo. 9Wala tusimjaribu Kristo, kama wengi wao walivyofanya na wakaharibiwa kwa nyoka. 10Na pia msinung'unike, kama wengi wao walivyonung'unika na kuharibiwa na malaika wa mauti. 11Basi mambo hayo yalitendeka kama mifano kwetu. Yakaandikwa ili kutuonya sisi - tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 12Kwa hiyo kila ajionaye amesimama awe makini asije akaanguka.

Injili

Mt 16:6–12

6Yesu akawaambia “ Jitahadharini na iweni makini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” 7Wanafunzi wakahojiana miongoni mwao na kusema. “Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.” 8Yesu alitambua hilo na kusema, “Enyi wenye imani ndogo, kwa nini mmewaza na kusemezana miongoni mwenu na kusema kuwa ni kwa sababu hamkuchukua mikate? 9Je bado hamtambui wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa watu elfu tano, na vikapu vingapi mlivyokusanya? 10Au mikate saba kwa watu elfu nne, na ni vikapu vingapi mlikuchukua? 11Imekuwaje kuwa hata hamuelewi ya kuwa nilikuwa sizungumzi nanyi juu ya mikate? Jitunzeni na jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.” 12Kisha wakatambua kuwa alikuwa hawaambii juu ya kujihadhari na mikate iliyo na chachu, bali kujihadhari na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 10 Agosti

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 28 Julai katika kalenda ya kanisa ni 10 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki