Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 6 Agosti
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 6 Agosti 2027
Ijumaa · Juma la 18 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Kugeuka Sura kwa Bwana
Sikukuu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Kufunga na toba
Siku ya toba
Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.
Masomo ya siku
Somo la kwanza
au: 2 Pet 1:16–19
9Na nilipotazama, viti vya enzi vilikuwa vimewekwa, na Mtu wa siku za kale alikaa sehemu yake. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theruji, na nywele zake katika kichwa chake zilikuwa safi kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa na miali ya moto, na magurudumu yake yalikuwa yanawaka moto. 10Mto wa moto ulitiririka kutoka mbele yake, na mamilioni ya watu walimtumikia, na wengine mia moja milioni walikuwa wamesimama mbele yake. Na mahakama iliitishwa, na vitabu vilifunguliwa. 13Katika maono yangu usiku ule, nilimwona mtu mmoja anakuja katika mawingu ya mbinguni alikuwa kama mwana wa mtu; alikuja kwa Mzee wa Siku na aliletwa mbele zake. 14Naye alipewa mamlaka ya kiutawala na utukufu na mamlaka ya kifalme ili kwamba watu wote, na mataifa na lugha ziweze kumtumikia yeye. Mamlaka yake ya kutawala ni mamlaka ya milele ambayo hayatapita, na ufalme wake ni ule ambao hautaangamizwa.
Wimbo wa katikati
1Yahwe anatawala; nchi ishangilie; visiwa vingi na vifurahi. 2Mawingu na giza vyamzunguka. Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake. 5Milima huyeyuka kama nta mbele za Yahwe, Bwana wa dunia yote. 6Mbingu hutangaza haki yake, na mataifa yote huuona utukufu wake. 9Kwa kuwa wewe, Yahwe, ndiye uliye juu sana, juu ya nchi yote. Umetukuka sana juu ya miungu yote.
Injili
2Na baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana pamoja naye mlimani, pekee yao. Ndipo alianza kubadilika mbele yao. 3Mavazi yake yakaanza kung'aa sana, meupe zaidi, meupe kuliko mng'arishaji yeyote duniani. 4Ndipo Eliya pamoja na Musa walitokea mbele yao, na walikuwa wakiongea na Yesu. 5Petro alijibu akamwambia Yesu, “Mwalimu, ni vyema sisi kuwa hapa, na tujenge vibanda vitatu, kimoja kwa ajili yako, kimoja kwa ajili Musa na kingine kwa ajili ya Eliya.” 6(Kwa kuwa hakujua nini cha kusema, waliogopa sana.) 7Wingu lilitokea na kuwafunika. Ndipo sauti ikatoka mawinguni ikisema, “ Huyu ni mwanangu mpendwa. Msikieni yeye.” 8Ghafla, walipokuwa wakitazama, hawakumuona yeyote pamoja nao, isipokuwa Yesu tu. 9Walipokuwa wanateremka kutoka mlimani, aliwaamuru kutokumwambia mtu yeyote yale yote waliyoyaona, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka kwa wafu.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki