Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 2 Agosti

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 2 Agosti 2027

Jumatatu · Juma la 18 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatatu ya Juma la 18 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Eusebi wa Vercelli, askofu · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Petro Yuliani Eymard, padre · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Hesabu 11:4–15

4Baadhi ya wageni wakaanza kuweka kambi zao pamoja na wana wa wa Israeli. Walitaka kula chakula kizuri. Kisha wana wa Israeli walipoanza kulia wakisema, “Ni nani atakayetupatia nyama za kula? 5Tunakumbuka samaki tulizokula bure kule Misri, yale matango, na matikiti maji, na mboga na vitunguu na vitunguu saumu. 6Na sasa hatuna hamu ya kula, kwa sababu tunaona mana tu. 7Mana ilifanana na punje ya mtama. ilionekana kama bedola. 8watu wakazunguka kisha wakakusanyika. Wakaisaga, wakaitwanga kwa vinu, wakaitokosa nyunguni, na kuitengeneza mikate. radha yake ilikuwa kama mafuta mapya ya mizeituni. 9Na umande ulipoanguka kambini usiku ule, na mana ilianguka pia. 10Musa akawasikia watu wakilia katika familia zao, na kila mtu alikuwa kwenye lango la hema yake. BWANA alikasirika sana, na mbele ya macho ya Musa malalamiko yao yalikuwa mabaya. 11Musa akasema na BWANA, “Kwa nini umemtendea mtumishi wako vibaya namna hiyo? kwa nini hujapendezwa na mimi? unanifanya kubeba mizigo ya hawa watu. 12Je, mimi ndiye niliyewatungia mimba hawa watu? Mimi ndiye niliyewazaa kiasi kwamba unaniambia, “wabebe kwa ukaribu vifuani mwako kama baba abebavyo mtoto wake? Je, nitawabeba mpaka kwenye nchi ambayo uliwaahidi mababu zao kuwapa? 13Naweza kupata wapi nyama za kuwapa watu wote hawa? Wanalia mbele zangu na wanasema, 'tupe nyama tule.' 14Mimi peke yangu siwezi kuwabeba watu wote hawa. Ni wengi sana kwangu. 15Kwa vile unanitendea hivi, basi uniue, na kama wewe ni mpole kwangu, basi niondolee mzigo huu.”

Wimbo wa katikati

Zab 81:11–16

11Lakini watu wangu hawakusikiliza maneno yangu; Israeli hawakunitii. 12Nikawaacha waende katika katika njia yao wenyewe ya ukaidi ili kwamba waweze kufanya kinachoonekana sahihi kwao. 13Oh, laiti watu wangu wangenisikiliza mimi; oh, watu wangu wangelitembea katika njia yangu. 14Kisha ningewatiisha adui zao haraka na kugeuzia mkono wangu dhidi ya watesi wao. 15Wale wanaomchukia Yahwe katika hofu na waanguke chini mbele zake! Wawe wanyonge milele. 16Ningewalisha Israeli kwa ngano bora; Ningewatosheleza kwa asali itokayo mwambani.”

Injili

Mt 14:13–21

13Naye Yesu aliposika haya, akijatenga kutoka mahali pale akapanda ndani ya mashuka akaenda sehemu iliyotengwa. Wakati umati ulipo fahamu alikokuwa, walimfuata kwa miguu kutoka mijini. 14Kisha Yesu alikuja mbele yao akauona umati mkubwa. Akawaonea huruma na kuponya magonjwa yao. 15Jioni ilipotimia, wanafunzi wakaja kwake na kusema, “Hii ni sehemu ya jangwa, na siku tayari imepita. Watawanyishe makutano ili waende vijijini wakanunue chakula kwa ajili yao. 16Lakini Yesu akawaambia, ''Hawana haja ya kwenda zao. Wapeni ninyi chakula” 17Wakamwambia, ''Hapa tunayo mikate mitano na samaki wawili tu.”'' 18Yesu akasema, “Ileteni kwangu.” 19Kisha Yesu akauamuru umati kukaa chini ya nyasi. Akachukuwa mikate mitano na samaki wawili. Akatazama juu mbinguni, akabariki na kumega mikate akawapa wanafunzi. Wanafunzi wakaupatia umati. 20Wakala wote na kushiba. Kisha wakavikusanya vipande vyote vya chakula na kujaza vikapu kumi na mbili. 21Wale waliokula walikadiriwa kuwa wanaume elfu tano bila ya kusehabu wanawake na watoto.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 2 Agosti

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki