Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 31 Julai
Kalenda ya Kiorthodoksi · 18 Julai (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 31 Julai 2027
Jumamosi · Wiki ya 6 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Mfiadini Hiasintho wa Amastri (karne ya 4)
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Nasema ukweli katika Kristo. Sisemi uongo, na dhamira yangu hushuhudia pamoja nami katika Roho Mtakatifu, 2kwamba kuna huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma ndani ya moyo wangu. 3Kwamba ningetamani mimi mwenyewe kulaaniwa na kutengwa mbali na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, wale wa jamii yangu katika mwili. 4Wao ni Waisraeli. Walio na hali ya kufanyika watoto, wa utukufu, wa maagano, na zawadi ya sheria, kumwabudu Mungu, na ahadi. 5Wao ni watangulizi ambako Kristo amekuja kwa heshima kuvaa mwili huu - ambaye yeye ni Mungu wa vyote. Naye asifiwe milele. Amina.
Injili
18Wakati Yesu alipokuwa akiwaambia mambo hayo, tazama, afisa akaja akasujudu mbele yake, Naye akasema, “ Binti yangu amefariki punde, lakini njoo na uweke mkono wako juu yake na yeye ataishi tena. 19Ndipo Yesu akasimama na kumfuata na wanafunzi wake pia. 20Tazama, mwanamke ambaye alikuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja karibu na Yesu na akagusa sehemu ya pindo la vazi lake. 21Kwa kuwa alisema, “Endapo nitagusa vazi lake, nami nitapata uponyaji.” 22Yesu akageuka na kumtazama na kumwambia. “Binti, jipe moyo, imani yako imekufanya upone,” Na muda huo huo mwanamke akapata uponyaji muda huo. 23Na Yesu alipofika kwenye nyumba ya afisa, naye aliwaona wapiga tarumbeta na umati wa watu ulikuwa ukipiga kelele. 24Naye akasema, “Tokeni hapa, kwa kuwa binti hajafa, bali amelala. Lakini wao walicheka na kumkebehi. 25Na wale watu walipotolewa nje, naye akaingia chumbani na kumshika mkono na msichana akaamka. 26Na habari hizi zikaenea katika mji mzima.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Emiliani (363)
- Mtawa Mfiadini Apolinari (1918)
- Mtakatifu Mtawa Pambo, mkaa jangwani (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Yohana, aliyeteseka sana, wa Mapango ya Kyiv (1160)
- Mtakatifu Mtawa Pambo, mtawa wa faragha wa Mapango ya Kyiv (karne ya 13)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 18 Julai katika kalenda ya kanisa ni 31 Julai katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki