Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 31 Julai

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 31 Julai 2027

Jumamosi · Juma la 17 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 17 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Ignasi wa Loyola, padre · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Law 25:1, 8–17

1Yahweh akazungumza na Musa kwenye Mlima wa Sinai, akisema, 8Ni lazima kwenu kuhesabu Sabato saba za miaka, yaani, saba mara miaka saba, ikifanya jumla ya miaka arobaini na tisa. 9Kisha mtapiga sauti ya tarumbeta kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho ni lazima mtapiga tarumbeta katika nchi yenu yote. 10Nanyi mtautenga mwaka wa hamsini kwa ajili ya Yahweh na mtatangaza uhuru katika nchi yote kwa wakazi wote. Kutakuwa na Yubile kwa ajili yenu, ambayo kwayo mali na watumwa ni lazima warejeshwe kwa familia zao. 11Mwaka wa saba kutakuwa na Yubile kwenu. Hamtapanda wala kusimamia mavuno ya kijioteshacho chenyewe, na kukusanya kichipukacho kwenye mizabibu isiyokatiwa matawi. 12Kwa sababu hiyo ni Yubile takatifu kwenu. Nanyi mtakula mazao yanayokua yenyewe kutoka mashambani. 13Ni lazima muwarejeshe kila mmoja kwenye miliki yake katika mwaka huu wa Yubile. 14Iwapo utauza ardhi yoyote ya jirani yako au kununua ardhi yake, ni shrti msipunjane au kutendeana kwa hila. 15Iwapo unanunua ardhi kutoka kwa jirani yako, zingatia idadi ya miaka na mazao ambayo yaweza kuvunwa mpaka mwaka wa Yubile nyingine. Jirani yako anayeuza ardhi ni lazima aihesabu miaka hiyo pia. 16Miaka inapoongezeka mpaka Yubile nyingine, ataongeza thamani ya ardhi, na miaka inapokuwa michache kufikia Yubile nyingine atashusha thamani, kwa sababu idadi ya mavuno inahusiana na idadi ya miaka kabla ya Yubile nyingine. 17Msipunjane au kutendeana kwa hila, badala yake, yawapasa kumheshi Yahweh Mungu wenu.

Wimbo wa katikati

Zab 67:1–2, 4, 6–7

1Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. zaburi, wimbo. Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah 2ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote. 4Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani. 6Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki. 7Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.

Injili

Mt 14:1–12

1Kwa wakati huo, Herode alisikia habari juu ya Yesu.. 2Akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu. Kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake.” 3Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake. 4Kwa kuwa Yohana alimwambia, “Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake.” 5Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii. 6Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode. 7Katika kujibu kili aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba. 8Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, “Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.” 9Mfalme alikuwa na sikitiko kwa maombi ya binti, lakini kwa ajili ya kiapo chake, kwa sababu ya wote waliokuwa chakulani pamoja naye aliamuru kwamba inapaswa ifanyike. 10Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani 11ili akatwe kichwa chake na kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti na akakipeleka kwa mama yake. 12Kisha wanafunzi wake wakaja kuuchukua ule mwili na kuuzika, baada ya hili walienda kumwambia Yesu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 31 Julai

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki