Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 30 Julai

Kalenda ya Kiorthodoksi · 17 Julai (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 30 Julai 2027

Ijumaa · Wiki ya 6 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4

Sikukuu na watakatifu

Mfiadini Mkuu Marina (Margareta) (karne ya 4)

Siku ya mfungo

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

1 Kor 4:5–8

5Kwa hiyo, msitamke hukumu juu ya lolote kabla ya wakati, kabla ya kuja kwa Bwana. Atayaleta nuruni mambo yaliyofichika gizani na kufunua makusudi ya mioyo. Ndipo kila mmoja atapokea sifa yake kutoka kwa Mungu. 6Sasa, kaka na dada zangu, mimi mwenyewe na Apolo nimetumia kanuni hizi kwa ajili yenu. Ili kwamba kutoka kwetu mnaweza kujifunza maana ya usemi, “Usiende zaidi ya kilivyoandikwa.” Hii ni kwamba hakuna mmoja wenu ajivunaye juu ya mwingine. 7Maana ni nani aonaye tofauti kati yenu na mwingine? Ni nini ulicho nacho hukukipokea bure? Kama umekwisha kupokea bure, kwa nini mnajivuna kama hamkufanya hivyo? 8Tayari mnavyo vyote ambavyo mngetaka! Tayari mmekuwa na utajiri! Mmeanza kutawala-na kwamba mnamiliki zaidi yetu sisi! Kweli, nawatakia umililki mwema ili kwamba tumiliki pamoja nanyi.

Injili

Mt 13:44–54

44Ufalme wa mbinguni ni kama hazina iliyofichwa shambani. Mtu akaiona na kuificha. Katika furaha yake akaenda kuuza vyote alivyokuwa navyo, na kulinunua shamba. 45Tena, ufalme wa mbinguni ni kama mtu anayefanya biashara atafutaye lulu yenye thamani. 46Wakati alipoiona ile yenye thamani, alienda akauza kila kitu alichokuwa nacho na akainunua. 47Ufalme wa mbinguni ni kama nyavu iliyo ndani ya bahari, na kwamba hukusanya viumbe vya kila aina. 48Ulipojaa wavuvi waliuvuta ufukweni. Kisha wakakaa chini wakakusanya vitu vyema ndani ya vyombo, lakini visivyo na thamani vilitupwa mbali. 49Itakuwa namna hii katika mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenga watu waovu kutoka miongoni mwa wenye haki. 50Na kuwatupa ndani ya tanuru ya moto, ambako kutakuwa na maombolezo na kusaga meno. 51Mmefahamu mambo yote haya? Wanafunzi walimjibu, ''Ndiyo.'' 52Kisha Yesu akawambia, ''Kila mwandishi ambaye amekuwa mwanafunzi wa ufalme anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.'' 53IkawaYesu alipomaliza mifano yote hiyo, akaondoka katika sehemu hiyo. 54Kisha Yesu akafika katika mkoa wake na akawafundisha watu katika sinagogi. Matokeo yake ni kuwa walishangaa na kusema, “Ni wapi mtu huyu alipopata hekima hii na miujiza hii?

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 30 Julai

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 17 Julai katika kalenda ya kanisa ni 30 Julai katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki