Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 29 Julai

Kalenda ya Kiorthodoksi · 16 Julai (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 29 Julai 2027

Alhamisi · Wiki ya 6 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4

Sikukuu na watakatifu

Mfiadini wa Kikasisi Athenogeni, askofu, na wanafunzi wake kumi (karibu 311)

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

1 Kor 3:18–23

18Mtu asijidanganye mwenyewe, kama yeyote miongoni mwenu anadhani ana hekima katika nyakati hizi, awe kama “mjinga” ndipo atakuwa na hekima. 19Kwa kuwa hekima ya dunia hii ni ujinga mbele za Mungu, Kwa kuwa imeandikwa, “Huwanasa wenye hekima kwa hila zao” 20Na tena “Bwana anajua mawazo ya wenye busara ni ubatili.” 21Hivyo mtu asijivunie wanadamu! Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu. 22Kama ni Paulo, au Apolo, au Kefa, au dunia, au maisha, au kifo, au vitu vilivyopo, au vitakavyokuwepo. Vyote ni vyenu, 23na ninyi ni wa Kristo na Kristo ni wa Mungu.

Injili

Mt 13:36–43

36Kisha Yesu aliwaacha makutano na kwenda nyumbani. Wanafunzi wake walimwendea na kusema, “Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani.'' 37Yesu alijibu na kusema, “Apandae mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu. 38Shamba ni ulimwengu; na mbegu nzuri, hawa ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu, na adui aliye zipanda ni ibilisi. 39Na mavuno ni mwisho wa ulimwengu, na wavunaji ni malaika. 40Kama vile magugu yanavyo kusanywa na kuchomwa moto, hivyo ndivyo itakavyo kuwa mwisho wa ulimwengu. 41Mwana wa Adamu atatuma malaika wake, na kukusanya kutoka katika ufalme wake mambo yote yaliyosababisha dhambi na wale watendao maasi. 42Watawatupa wote katika tanuru la moto, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 43Ndipo watu wenye haki watakapong'aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio na sikie.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 29 Julai

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 16 Julai katika kalenda ya kanisa ni 29 Julai katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki