Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 25 Julai

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 25 Julai 2027

Jumapili · Juma la 17 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Dominika ya 17 ya Mwaka

Dominika · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

2 Fal 4:42–44

42Akaja mtu kutoka Baal Shalisha kwa mtu wa Mungu na kumletea chakula cha kwanza cha mavuno yake mikate shirirni ya shayiri, na masuke mabichi kwenye gunia. Akasema, “Wape haya watu ili waweze kula.” 43Mtumishi wake akasema, “Je, niandae hii mbele ya watu mia moja?” Lakini Elisha akasema, “Wapeni hawa watu, ili waweze kula, kwa sabau Yahwe anasema, 'Watakula na kingine kitabaki.”' 44Basi mtumishi wake akawaandalia mbele yao; wakala, na kuacha kingine kimebaki, kama neno la Yahwe lilivyokuwa limesema.

Wimbo wa katikati

Zab 145:10–11, 15–18

10Vyote ulivyo viumba vitakushukuru wewe, Yahwe; waaminifu wako watakutukuza wewe. 11Waaminifu wako watanena juu ya utukufu wa ufalme wako, na watahubiri juu ya nguvu zako. 15Macho ya wote yanakungoja wewe; nawe huwapa chakula chao kwa wakati sahihi. 16Huufungua mkono wako na hukidhi haja ya kila kiumbe hai. 17Yahwe ni mwenye haki katika njia zake zote na neema katika yote afanyayo. 18Yahwe yu karibu na wote wamwitao, wale wamwitao yeye katika uaminifu.

Somo la pili

Efe 4:1–6

1Kwa hiyo, kama mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mtembee sawasawa na wito ambao Mungu aliwaita. 2Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo. 3Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4Kuna mwili mmoja na Roho moja, kama ambavyo pia mlikuwa mmeitwa katika uhakika wa taraja moja la wito wenu. 5Na kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, 6na Mungu mmoja na Baba wa wote. Yeye yuko juu ya yote, na katika yote na ndani ya yote.

Injili

Yn 6:1–15

1Baada ya mambo haya, Yesu alienda pande za Bahari ya Galilaya, pia huitwa Bahari ya Tiberia. 2Mkutano mkubwa ulikuwa ukimfuata kwa sababu waliona ishara alizozifanya kwa waliokuwa wagonjwa. 3Yesu alipanda juu hadi upande wa juu wa mlima na akakaa huko na wanafunzi wake 4(Na Pasaka, Sikukuu ya Wayahudi ilikuwa imekaribia). 5Yesu alipoinua macho yake juu na kuona umati mkubwa unakuja kwake, akamwambia Filipo, “Tutakwenda wapi kununua mikate ili hawa waweze kula”? 6(Lakini Yesu aliyasema haya kwa Filipo kwa kumjaribu kwa kuwa yeye mwenyewe alijua atakachofanya). 7Filipo akamjibu, “Hata mikate ya thamani ya dinari mia mbili isingelitosha hata kila mmoja kupata hata kipande kidogo.” 8Andrea, mmoja wa wanafunzi wake ndugu yake Simoni Petro akamwambia 9Yesu, “Kuna mvulana hapa ana mikate mitano na samaki wawili, lakini hii yafaa nini kwa watu wengi namna hii?” 10Yesu akawambia, “Waketisheni watu chini” (kulikuwa na nyasi nyingi mahali pale). Hivyo wanaume wapata elfu tano wakakaa chini. 11Kisha Yesu akachukua ile mikate mitano akashukuru akawawagawia wale waliokuwa wamekaa. Vivyo hivyo akawagawia samaki kwa kadiri ya vile wavyohitaji. 12Watu waliposhiba, aliwambia wanafunzi wake, “Vikusanyeni vipande vya mabaki, vilivyobaki ili kwamba kisipotee chochote.” 13Basi wakakusanya na kujaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri- vipande vilivyosazwa na wale waliokula. 14Kisha watu walipoona ishara hii aliyoifanya walisema, “Kweli huyu ndiye yule nabii ajaye ulimwenguni.” 15Yesu alipotambua kuwa walikuwa wanataka kumkamata ili wamfanye kuwa mfalme wao, alijitenga, tena na akaenda mlimani yeye peke yake.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 25 Julai

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki