Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 19 Julai

Kalenda ya Kiorthodoksi · 6 Julai (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 19 Julai 2027

Jumatatu · Wiki ya 5 baada ya Pentekoste · Sauti ya 3

Sikukuu na watakatifu

Mtakatifu Mtawa Sisoe Mkuu (429)

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka

Rum 12:4–5, 15–21

4Kwa kuwa tuna viungo vingi katika mwili mmoja, lakini si viungo vyote vina kazi moja. 5Vivyo hivyo, sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake. 15Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia. 16Muwe na nia moja ninyi kwa ninyi. Msifikiri kwa kujivuna, lakini wakubalini watu wa hali ya chini. Msiwe na hekima juu ya mawazo yenu wenyewe. 17Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Fanyeni mambo mema machoni pa watu wote. 18Kama inawezekana, kama ilivyowekwa kwenu, muwe na amani na watu wote. 19Wapenzi, msijilipizie kisasi wenyewe, lakini ipisheni ghadhabu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, '' 'kisasi ni changu; Mimi nitalipa,' asema Bwana.” 20“Lakini ikiwa adui yako ana njaa, mlishe. Akiwa na kiu, mnyweshe. Kwa maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto juu ya kichwa chake.” 21Usishindwe na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.

Injili

Mt 12:9–13

9Kisha Yesu akatoka pale akaenda katika sinagogi lao. 10Tazama kulikuwa na mtu aliyepooza mkono. Mafarisayo wakamuuliza Yesu, wakisema. “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?” ili kwamba waweze kumshitaki kwa kutenda dhambi. 11Yesu akawaambia, “Nani kati yenu, ambaye ikiwa ana kondoo mmoja, na huyu kondoo akaanguka ndani ya shimo siku ya sabato, hatamshika na kumtoa kwa nguvu ndani ya shimo? 12Je, ni kipi chenye thamani, zaidi kwani, si zaidi ya kondoo! Kwa hivyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.'' 13Kisha Yesu akamwambia yule mtu,” Nyoosha mkono wako” Akaunyoosha, na ukapata afya, kama ule mwingine.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 19 Julai

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 6 Julai katika kalenda ya kanisa ni 19 Julai katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki