Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 18 Julai

Kalenda ya Kiorthodoksi · 5 Julai (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 18 Julai 2027

Jumapili · Sauti ya 3

Sikukuu na watakatifu

Jumapili ya 4 baada ya Pentekoste

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Sala ya Jioni: somo (Mt. Athanasio)

Haimo katika tafsiri hii

Sala ya Jioni: somo (Mt. Athanasio)

Haimo katika tafsiri hii

Sala ya Jioni: somo (Mt. Athanasio)

Haimo katika tafsiri hii

Sala ya Jioni: somo (Mt. Sergio)

Mit 10; Mit 3; Mit 8 (mistari iliyochaguliwa)

Sala ya Jioni: somo (Mt. Sergio)

Mit 10:31–11:12

31Katika kinywa cha wale watendao haki hutoka tunda la hekima, bali ulimi wa kupotosha utakatwa. 32Midomo ya wale watendao mema huyajua yanayokubalika, bali kinywa cha waovu, huyajua yanayopotosha. 11:1Yehova huchukia vipimo ambavyo havipo sahihi, bali hufurahia uzani dhahiri. 2Kinapokuja kiburi, ndipo aibu huja, bali unyenyekevu huleta hekima. 3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali udanganyifu wa njia za wajanja utawaangamiza. 4Utajiri hauna thamani siku ya ghadhabu, bali kwa kutenda haki hujilinda na mauti. 5Mwenendo wa mtu mwema huinyosha njia yake, bali waovu wataanguka kwa sababu ya uovu wao. 6Mwenendo mwema wa wale wampendezao Mungu utawalinda salama, bali wadanganyifu hunaswa katika shauku zao. 7Mtu mwovu anapokufa, tumaini lake hupotea na tumaini lililokuwa katika nguvu zake linakuwa si kitu. 8Yule atendaye haki hulindwa katika taabu na badala yake taabu humjia mwovu. 9Kwa kinywa chake asiyeamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa wale watendao haki hulindwa salama. 10Wanapofanikiwa watendao haki, mji hufurahi, waovu wanapoangamia, kunakuwa na kelele za furaha. 11Kwa zawadi nzuri za wale wanaompendeza Mungu, mji unakuwa mkubwa; kwa kinywa cha waovu mji huvurugwa. 12Mtu mwenye dharau kwa rafiki yake hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hunyamaza.

Sala ya Jioni: somo (Mt. Sergio)

Haimo katika tafsiri hii

Injili ya 4 ya Sala ya Alfajiri

Lk 24:1–12

1Mapema sana siku ya kwanza ya juma, walikuja kaburini, wakileta manukato ambayo walikuwa wameyaandaa. 2Wakakuta jiwe limevingirishwa mbali na kaburi. 3Wakaingia ndani, lakini hawakuukuta mwili wa Bwana Yesu. 4Ilitokea kwamba, wakati wamechanganyikiwa kuhusu hili, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi ya kung'aa. 5Wanawake wakiwa wamejaa hofu na wakiinamisha nyuso zao chini, wakawaambia wanawake, “Kwanini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? 6Hayupo hapa, ila amefufuka! Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa angali Galilaya, 7akisema kwamba Mwana wa Adamu lazima atolewe kwenye mikono ya watu wenye dhambi na asulubishwe, na siku ya tatu, afufuke tena.” 8Wale wanawake wakakumbuka maneno yake, 9na wakarudi kutoka kaburini na wakawaambia mambo haya yote wale kumi na moja na wengine wote. 10Basi Maria Magdalena, Joana, Maria mama wa Yakobo, na wanawake wengine pamoja nao wakatoa taarifa hizi kwa mitume. 11Lakini ujumbe huu ukaonekana kama mzaha tu kwa mitume, na hawakuwaamini wale wanawake. 12Hata hivyo Petro aliamka, na akakimbia kuelekea kaburini, na akichungulia na kuangalia ndani, aliona sanda peke yake. Petro kisha akaondoka akaenda nyumbani kwake, akistaajabu nini ambacho kimetokea.

Waraka

Rum 6:18–23

18Mmefanywa huru kutoka kwenye dhambi, na mmefanywa watumwa wa haki. 19Ninazungumza kama mtu kwa sababu ya madhaifu ya miili yenu. Kwa maana kama vile mlivyotoa viungo vya miili yenu kuwa watumwa kwa uchafu na uovu, kwa jinsi iyo hiyo, sasa toeni viungo vya miili yenu kuwa watumwa wa haki kwa utakaso. 20Kwa kuwa mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. 21Kwa wakati huo, mlikuwa na tunda lipi kwa mambo ambayo kwa sasa mnaona aibu kwayo? Kwa kuwa matokeo ya mambo hayo ni kifo. 22Lakini kwa kuwa sasa mmefanywa huru mbali na dhambi na mmefanyika watumwa kwa Mungu, mna tunda kwa ajili ya utakaso. Tokeo ni uzima wa milele. 23Kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, bali zawadi ya bure ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Waraka (mmojawapo wa watakatifu)

Gal 5:22–6:2

22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani, 23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo. 24Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya. 25Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho. 26Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu. 6:1Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe. 2Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.

Injili

Mt 8:5–13

5Wakati Yesu alipofika Kapernaumu, Jemedari akaja kwake akamuuliza 6akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza na ana maumivu ya kutisha.” 7Yesu akamwambia, “Nitakuja na kumponya”. 8Jemedari akajibu na kumwambia, “Bwana, mimi si wathamani hata uje na kuingia ndani ya dari yangu, sema neno tu na mtumishi wangu ataponywa. 9Kwa kuwa mimi pia ni mtu niliye na mamlaka, na ninao askari walio chini yangu. Nikisema kwa huyu “Nenda' na huenda, na kwa mwingine 'Njoo' na yeye huja, na kwa mtumishi wangu, 'Fanya hivi,' na yeye anafanya hivyo” 10Wakati Yesu aliposikia haya, alishangazwa na kuwaambia wale waliokuwa wakimfuata, “Kweli ninawaambia, Sijapata kuona mtu mwenye imani kama huyu katika Israel. 11Ninawambieni, wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, wataketi katika meza pamoja na Abrahimu, Isaka, na Yakobo, katika ufame wa mbinguni. 12Lakini watoto wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambapo kutakuwa na kilio na kusaga meno.” 13Yesu akamwambia Jemadari, “Nenda! Kama ulivyokwisha amini, na itendeke hivyo kwako”. Na mtumishi aliponywa katika saa hiyo.

Injili (mmojawapo wa watakatifu)

Lk 6:17–23

17Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. 18Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia. 19Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote. 20Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu. 21Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka. 22Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu. 23Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 18 Julai

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 5 Julai katika kalenda ya kanisa ni 18 Julai katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki