Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 24 Juni

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 24 Juni 2027

Alhamisi · Juma la 12 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Kuzaliwa kwa Mt. Yohane Mbatizaji

Sherehe · Rangi ya liturujia: nyeupe

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Isa 49:1–6

1Nisikilize mimi, enyi mkao pwani! na kuwa makini, enyi watu mkao mbali. Yahwe amenita mimi kutoka kuzaliwa kwa jina, mama yangu aliponileta duniani. 2Amefanya mdomo wangu kuwa kama upanga mkali; amenificha mimi katika kivuli cha mkono wake; amenifanya mimi kuwa mshale unaong'aa; katika podo yake amenificha mimi. 3Amesema na mimi, ''Wewe ni mtumishi wangu, Israeli, kupitia yeye nitaonyesha utukufu wangu.'' 4Lakini nilimjibu, ''Japo nilifikiria nilifanya kazi bure, nimetumia nguvu zangu bure, ikiwa haki yangu iko pamoja na Yahwe, na zawadi yangu iko kwa Mungu wangu. 5Na sasa Yahwe asema hivi, yeye aliyeniumba mimi toka kuzaliwa na kuwa mtumishi wake, kumrejesha Yakobo tena kwake mwenyewe, na Israeli wakusanyike kwake. Mimi ninaheshimika katika macho ya Yahwe, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu. 6Asema hivi, ''Ni kitu kidogo sana kwa wewe kuwa mtumishi wangu ili kuanzisha ukoo wa Yakobo, na kuwarejesha wanaoishi Israeli. Nitakufanya wewe kuwa mwanga kwa Wayunani, ili uwe wokovu wangu katika mipaka ya nchi.

Wimbo wa katikati

Zab 139:1–3, 13–15

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya daudi. Ee Yahwe, wewe umenichunguza, na unanijua. 2Wewe unajua nikaapo na niinukapo; unayajua mawazo yangu tokea mbali sana. 3Unachunguza wenendo wangu na kulala kwangu; unazijua njia zangu zote. 13Wewe uliumba sehemu zangu za ndani; uliniumba tumboni mwa mama yangu. 14Nitakusifu, kwa maana nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu. Nafsi yangu yalijua hili vizuri sana. 15Mifupa yangu haikusitirika kwako nilipoumbwa kwa siri, nilipoumbwa kwa ustadi pande za chini za nchi.

Somo la pili

Mdo 13:22–26

22Kisha baada ya Mungu kumuondoa katika ufalme, alimwinua Daudi kuwa mfalme wao. Ilikuwa ni kuhusu Daudi kwamba Mungu alisema, 'Nimempata Daudi mwana wa Yese kuwa mtu apendezwaye na moyo wangu; ambaye atafanya kila kitu nipendacho.' 23Kutoka kwenye ukoo wa mtu huyu Mungu ameiletea Israeli mkombozi, Yesu, kama alivyoahidi kufanya. 24Hili lilianza kutokea, kabla ya Yesu kuja, Yohana kwanza alitangaza ubatizo wa toba kwa watu wote wa Israeli. 25Naye Yohana alipokuwa akimalizia kazi yake, alisema, 'Mwanifikiri mimi ni nani? mimi si yule. Lakini sikilizeni, ajaye nyuma yangu, sisitahili kulegeza viatu vya miguu yake.' 26Ndugu, watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wale ambao kati yenu mnamwabudu Mungu, ni kwa ajili yetu kwamba ujumbe huu wa ukombozi umetumwa.

Injili

Lk 1:57–66, 80

57Sasa wakati ulikuwa umewadia kwa Elizabeti kujifungua mtoto wake na akajifungua mtoto wa kiume. 58Jirani zake na ndugu zake walisikia jinsi Bwana alivyoikuza rehema kwake, na wakafurahi pamoja naye. 59Sasa ilitokea siku ya nane kwamnba walikuja kumtahiri mtoto. Ingewapasa kumwita jina lake, “Zekaria,” kwa kuzingatia jina la baba yake, 60Lakini mama yake akajibu na kusema, “Hapana; ataitwa Yohana.” 61Wakamwambia, hakuna hata mmoja katika ndugu zako anayeitwa kwa jina hili.” 62Wakamfanyia ishara baba yake kuashiria yeye alitaka jina aitwe nani. 63Baba yake akahitaji kibao cha kuandikia, na akaandika, “Jina lake ni Yohana.” Wote wakashangazwa na hili. 64Ghafla mdomo wake ukafunguliwa na ulimi wake ukawa huru. Akaongea na kumsifu Mungu. 65Hofu ikawajia wote walioishi karibu nao. Mambo haya yakaenea katika nchi yote ya vilima vya Yudea. 66Na wote walioyasikia wakayatunza mioyoni mwao, wakisema, “ Mtoto huyu kuwa wa namna gani?” Kwasababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye. 80Sasa, yule mtoto akakua na kuwa mwenye nguvu rohoni na alikaa nyikani mpaka siku ya kujitokeza kwake kwa Israeli.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 24 Juni

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki