Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 8 Juni
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 8 Juni 2027
Jumanne · Juma la 10 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 10 la Mwaka
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
18Lakini kama vile Mungu alivyo mwaminifu, hatusemi vyote “Ndiyo” na “Hapana.” 19Kwa kuwa mwana wa Mungu, Yesu Kristo, ambaye Silvano, Timotheo na mimi tulimtangaza miongoni mwenu, siyo “Ndiyo” na “Hapana.” Badala yake, yeye wakati wote ni “Ndiyo.” 20Kwa kuwa ahadi zote za Mungu ni “Ndiyo” katika yeye. Hivyo pia kupitia yeye tunasema “Amina” kwa utukufu wa Mungu. 21Sasa ni Mungu ambaye hututhibitisha sisi pamoja nanyi katika Kristo, na alitutuma sisi. 22Aliweka muhuri juu yetu na alitupa Roho katika mioyo yetu kama dhamana ya kile ambacho angetupatia baadaye.
Wimbo wa katikati
129Sheria zako ni za ajabu, ndiyo sababu ninazitii. 130Ufafanuzi wa maneno yako huleta nuru; na kumpa ufahamu mjinga. 131Ninafungua kinywa changu na kutweta, maana ninazitamani amri zako. 132Unigeukie na unihurumie, kama ufanyavyo siku zote kwa wale walipendao jina lako. 133Uziongoze hatua zangu kwa neno lako; usiruhusu dhambi yeyote initawale. 135Uso wako umwangazie mtumishi wako, na unifundishe sheria zako.
Injili
13Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini kama chumvi imepoteza ladha yake, itawezaje kufanyika chumvi halisi tena? Kamwe haiwezi kuwa nzuri kwa kitu kingine chochote tena, isipokuwa ni kutupwa nje na kukanyagwa na miguu ya watu. 14Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojegwa juu ya mlima haufichiki. 15Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya kikapu, bali kwenye kinara, nayo yawaangaza wote walio ndani ya nyumba. 16Acha nuru yenu iangaze mbele za watu kwa namna ambayo kwamba, wayaone matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki