Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 2 Juni
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 2 Juni 2027
Jumatano · Juma la 9 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatano ya Juma la 9 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Watakatifu Marselino na Petro, mashahidi · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
2Mungu wangu, ninaamini katika wewe. Usiniache niaibishwe; usiwaache maadui zangu wafurahie ushindi wao kwangu. 3Asiaibishwe mtu yeyote anaye kutumaini bali waaibishwe wale watendao hila bila sababu! 4Unijulishe njia zako, Yahwe; unifundishe njia zako. 5Uniongoze kwenye kweli yako na unifundishe, kwa kuwa wewe ni Mungu wa wokovu wangu; ninakutumainia wewe siku zote za maisha yangu. 6Kumbuka, Yahwe, matendo yako ya huruma na uaminifu wa agano lako; kwa kuwa vimekuwapo siku zote. 7Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala uasi wangu; Uniweke akilini mwako pamoja na uaminifu wa agano kwa zababu ya uzuri wa wako, Yahwe! 8Yahwe ni mzuri na mwenye haki; kwa hiyo yeye huwafundisha njia mwenye dhambi. 9Yeye huwaelekeza wanyenyekevu kwa kile kilicho sahihi na yeye huwafundisha wao njia yake.
Injili
18Kisha Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, walimwendea. Wakamuwuliza, wakisema, 19“Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, 'Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.' 20Kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza alitwaa mke na kisha akafa, hakuacha watoto. 21Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika. 22Na wa saba alikufa bila kuacha watoto. Mwishowe na mwanamke pia akafa. 23Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, Je! Atakuwa mke wa nani? Kwani wale ndugu wote saba walikuwa waume wake.” 24Yesu aliwaambia, “Je! Hii si sababu kuwa mmepotoshwa, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?” 25Wakati wa kufufuka toka kwa wafu, hawataoa wala kuingia katika ndoa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. 26Lakini, kuhusu wafu ambao wanafufuliwa, Je! Hamkusoma kutoka katika kitabu cha Musa, katika habari za kichaka, jinsi Mungu alivyosema na kumwambia, 'Mimi ni Mungu wa Abrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?' 27Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Ni dhahiri mmepotoka.”
Watakatifu wa siku
- Watakatifu Marselino na Petro, mashahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki