Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 1 Juni

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 1 Juni 2027

Jumanne · Juma la 9 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 9 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyekundu

Mt. Yustino, shahidi · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 112:1–2, 7–9

1Msifuni Yahwe. Amebarikiwa mtu yule anaye mtii Yahwe, apendezwaye sana na amri zake. 2Kizazi chake kitakuwa ni chenye nguvu duniani; kizazi cha mcha Mungu kitabarikiwa. 7Haogopi habari mbaya; ni jasiri, akimtumainia Yahwe. 8Moyo wake ni mtulivu, hana woga, mpaka aonapo ushindi dhidi ya watesi wake. 9Huwapa masikini kwa ukarimu; haki yake yadumu milele; atainuliwa kwa heshima.

Injili

Mk 12:13–17

13Kisha wakawatuma baadhi ya mafarisayo na maherodia kwake ili kumtega kwa maneno. 14Walipofika, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba hujali maoni ya yeyote na huonyeshi upendeleo kati ya watu. Unafundisha njia ya Mungu katika ukweli. Je! Ni haki kulipa kodi kwa Kaisari au la? Je! Twaweza kulipa au la? 15Lakini Yesu alijua unafiki wao na kuwaambia, “Kwa nini mnanijaribu? Nipeni dinari niweze kuitazama.” 16Wakaleta moja kwa Yesu, Akawaambia, “Je! ni sura ya nani na maandishi yaliyopo hapa ni ya nani? Wakasema, “Ya Kaisari.” 17Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vya Kaisari na Mungu vitu vya Mungu.” Wakamstaajabia.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 1 Juni

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki